Shafi Abdarah mwenye umri wa miaka 18 akimsaidia mama yake Rafael Mohamed kumuongoza njia wakati walipokuwa wakielekea kutafuta mahitaji ya kila
Rafael mwenye umri wa miaka 36 mwenye watoto wanne anasumbuliwa na uvimbe usoni ambao ameupata akiwa tayari mkubwa katika kuhangaikia matibabu ameweza kwenda katika hospitali za Lugara Ndanda Lindi lakini imeshindikana pia alikwenda katika hospitali ya Mkoa wa Lindi lakini madaktari walimwambia kuwa haiwezekani kutibiwa yeye kutokana na mishipa ambayo inaunganisha sehemu ya ufahamu.
Rafael ni Mkazi wa Kijiji cha Mnamba kata ya Nampa anaomba msaada wa hali na mali kwa wasamalia wema ambao wataguswa na ugonjwa huo unaomsumbua kiasi cha kuhatalisha maisha yake anashindwa kuihudumia familia yake kutokana na matatizo hayo tayari anafamilia ya watoto 4.
Anaomba wasamalia wema wamsaidia kufanikisha safari yake ya kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi wa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwani tangu apate ungonjwa huo mwaka 1984 hadi hivi sasa amekwenda katika hospitali ya Lindi tu hii ni kutokana na yeye kukosa uwezo wa kifedha na mtu wa kumsaidia,alisema angependa pia kuona mashirika ya kidini na wadau wengine wakimsaidia ili kuokoa uhai wake ambao sasa upo mashakani.
Baadhi ya watu wamekuwa wakimuahidi kumsaidia kiasi cha kumpiga picha lakini haoni msaada wowote kutoka kwa watu hao.
Kuanzia mwaka 2006 ungonjwa huo umekua ukikuwa kwa kasi kiasi cha kufanya uvimbe uzibe macho na kumfanya awe kipofu, kwa upande mwingine anamuomba Mbunge wake wa jimbo lake la Mtama Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe aweze kumsaidia kwa tatizo lake hilo.
MSADA WA MATIBABU : Mwanafunzi wa shule ya msingi Nyagao ya wasioona na wanaoona, iliyopo Wilaya ya Lindi, akimsikiliza Rafael Mohamed,na mmoja wa mabibi wasioona wakati walipofika katika shule hiyo ambapo kulikuwa na hafala fupi ya kukabidhiwa vyakula na misaada mingingine iliyotolewa na Kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia kitengo chake cha Vodacom Foundation wakati wa Mfungo wa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment