Miongoni mwa washiriki wa Maonesho ya mwaka huu ya wiki ya Nenda kwa
Usalama ni Kampuni ya ASAS ambao mbali na shughuli za usafirishaji wa mizigo
pia ni wazalishaji wakubwa wa Bidhaa za Maziwa ambayo asilimia kubwa hupatikana
kutoka katika mashamba ya mifugo ya ASAS DAIRY FARM yaliyopo mkoani Iringa.
Ng’ombe wa kisasa, Mbuzi, kondoo, Ngamia na Farasi ni miongoni mwa mifugo
inayofugwa katika mashamba hayo.
Watoto ndio umri sahihi kutoa mafunzo ya namna
ya matumizi sahihi ya barabara. Na iwapo kama watoto hawa watapata elimu ya
kutosha juu ya utumiaji wa barabara itachangia kwa kiwango kikubwa yatachangia
kupunguza kiwango a ajali za barabarani miaka ijayo. Hapa watoto wakimsikiliza
ofisa wa Wizara ya Ujenzi.
.Wananchi
wa mjini Iringa wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa mmoja wa maofisa wa
Wizara ya Ujenzi walipotembelea katika banda hilo jana. Kauli mbiu ya
Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO,
ZINGATIA SHERIA”.
Mkurugenzi
Mkuu wa Makampuni ya ASAS, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wiki ya Nenda
kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed, akipokea cheti cha heshima kwa kuwa
wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali barabarani pamoja na
Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, kitaufa yanafanyika mkoani Iringa. (Picha na Mpigapicha wetu).
No comments:
Post a Comment