Mabingwa
wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) wakiwa na msafara wa watu 32
wanatarajia kuwasili nchini kesho (Desemba 19 mwaka huu). Timu hiyo
itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 11
kamili jioni kwa ndege ya PrecisionAir ikitokea Lusaka.
Mbali
ya wachezaji 24, msafara wa Zambia ambayo inakuja nchini kwa ajili ya
mechi dhidi ya Taifa Stars utakuwa na maofisa wengine wanane wakiwemo wa
benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Herve Renard aliyeipa timu hiyo
ubingwa wa Afrika mwaka jana nchini Gabon.
Wachezaji
kwenye msafara huo ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher
Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix
Katongo na Francis Kasonde.
Given
Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy
Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri,
Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack
Malambo na Stoppila Sunzu.
Mechi
dhidi ya Taifa Stars itafanyika Jumamosi (Desemba 22 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Dar es
Salaam tangu Desemba 12 mwaka huu chini ya Kocha Kim Poulsen kujiandaa
kwa mechi hiyo.
Viingilio
katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na
kijani, sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C,
sh. 20,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.
Tiketi
zinatarajiwa kuanza kuuzwa siku moja kabla ya mechi katika vituo vya
Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Uhuru, Mgahawa wa Steers
ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni Kariakoo, kituo cha mafuta cha
Ubungo OilCom na Dar Live Mbagala.
Pia
tiketi zitauzwa Ijumaa (Desemba 21 mwaka huu) kwenye tamasha la
Kilimanjaro Premium Lager kuhamasisha washabiki wa Taifa Stars
litakalofanyika kwenye viwanja vya Sigara, Chang’ombe.
ROBO FAINALI KOMBE LA UHAI KUPIGWA KESHO
Robo
Fainali za michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana
wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zitachezwa
kesho (Desemba 19 mwaka huu) kwenye viwanja vya Karume na Chamazi jijini
Dar es Salaam.
Mtibwa
Sugar itaumana na African Lyon kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
katika mechi itakayoanza saa 2 kamili asubuhi. Nazo Azam na JKT Ruvu
zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 2 kamili asubuhi.
Mechi
nyingine ya robo fainali itakuwa kati ya JKT Oljoro na Simba ambayo
itachezwa kuanzia saa 9 kamili alasiri kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume. Coastal Union na Ruvu Shooting zitacheza kwenye Uwanja wa
Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nusu
fainali ya michuano hiyo itachezwa Ijumaa ya Desemba 21 mwaka huu
Uwanja wa Chamazi, wakati fainali na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu
zitapigwa Jumapili ya Desemba 23 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume.
TWFA KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA MOROGORO
Uchaguzi
wa viongozi wapya wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania
(TWFA) unafanyika kesho (Desemba 19 mwaka huu) kwenye hoteli ya Midlands
mjini Morogoro.
Kamati
ya Uchaguzi ya TWFA ikiongozwa na Mama Ombeni Zavala ndiyo
itakayoendesha uchaguzi huo chini ya usimamizi wa Kamati ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Wagombea
katika uchaguzi huo ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy
wanaowania uenyekiti, Rose Kissiwa (mgombea pekee wa nafasi ya Makamu
Mwenyekiti), Amina Karuma na Cecilia Mkafum (wanawania ukatibu mkuu).
Wengine
ni Zena Chande (mgombea pekee wa nafasi ya Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF)
na Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya
Utendaji ya TWFA.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment