Mtiginjola
ambaye ni Wakili wa kujitegemea ataongoza kamati hiyo yenye wajumbe
watano ambayo sasa itakuwa chombo cha mwisho kusikiliza rufani
zinazotokana na uchaguzi wa TFF, na wanachama wa TFF ambao
hawatakubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Kabla
ya uteuzi huo, Mtiginjola alikuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya TFF
inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana. Nafasi
yake katika kamati hiyo na ile ya mjumbe mwingine Kamishna Msaidizi wa
Polisi (ACP) Shabani Semlangwa aliyefariki dunia Julai mwaka huu
zitajazwa hivi karibuni.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambayo vinara wake
(Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti) wanatakiwa kitaaluma kuwa wanasheria
ni Francis Kabwe. Kabwe ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Wajumbe
wengine walioteuliwa na Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake
cha jana (Desemba 23 mwaka huu) ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP),
Mohamed Mpinga ambaye pia kitaaluma ni Mwanasheria.
Wengine
ni mshambuliaji wa zamani wa timu ya Reli Morogoro, Profesa Madundo
Mtambo ambaye kwa sasa ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoine (SUA) kilichopo mjini Morogoro, na mdau wa soka Murtaza Mangungu
ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini.
MECHI YA STARS, CHIPOLOPOLO YAINGIZA MIL 109/-
Pambano
la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zambia
(Chipolopolo) lililochezwa juzi (Desemba 22 mwaka huu) limeingiza sh.
109,197,000.
Fedha
hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 17,383 waliokata tiketi
kushuhudia mechi kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh.
20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) ni sh. 16,657,169.49, maandalizi ya mchezo sh.
55,339,510, tiketi sh. 5,803,900, ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa
sh. 2,350,000, Wachina (technical support) sh. 2,000,000, umeme sh.
300,000 na maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000.
Nyingine
ni bonasi kwa Taifa Stars sh. 13,826,313, asilimia 20 ya gharama za
mchezo sh. 2,504,022, asilimia 10 ya uwanja sh. 1,252,011, asilimia 5 ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 626,005 na asilimia 65 ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 8,138,070.
Mapato
ya mechi nyingine za Taifa Stars ilizocheza nyumbani mwaka huu yalikuwa
Taifa Stars vs Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC (Leopards)
iliyofanyika Februari 23 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sh.
32,229,000. Taifa Stars vs Msumbiji (Mambas) iliyochezwa Februari 29
mwaka huu sh. 64,714,000.
Taifa
Stars vs Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam iliingiza sh. 40,980,000. Taifa Stars vs Gambia
(The Scorpions) iliyochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam zilipatikana sh. 124,038,000 na Taifa Stars vs Kenya (Harambee
Stars) iliyofanyika Novemba 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza iliingiza sh. milioni 45.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment