Tuesday, March 27, 2012

ASKALI POLISI ASHINDA MILIONI 10 ZA M-PESA

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo. Katikati ni Ofisa Mkuu wa M-PESA Dylan Lenox. Jumla ya shilingi milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea ambayo inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 pindi mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.

NA MWANDISHI WETU DAR.
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom hivi karibuni il imkabidhi hundi mshindi wa zawadi ya kitita cha Shilingi Milioni Kumi wa droo ya mwezi ya promosheni ya M-PESA Bw Peter James Kilalo.

Bw. Kilalo amekabidhiwa hundi hiyo leo jijini Dra es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacoim Tanzania Bw. Rene Meza katika hafla fupi iliyohudhuriwa pia na waandishi wa habari.

Akipokea hundi yake Bw. Kilalo ambae ni Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Dar es salaam ameshukuru kw akuibuka mshindi jambo ambalo amesema hakulitegemea.

“Kwa kweli mimi ni mteja mzuri sana wa M-PESA lakini kweli sikutegemea kwamba ningeibuka mshindi, ila sasa ninapopokea hundi hii naamini kwamba nimeshinda na fedha hizi Milioni kumi ni zangu”Alibainisha Bw. Kilalo.

Alipoulizwa namna alivyojipanga kutumia pesa hizo Bw Kialalo alijibu” Jamani mimi ni masikini na sikuwahi kuota kwamba ipo siku nitashinda kiasi kikubwa cha fedha namna hii hivyo jambo kubwa kwangu kwa wakati huu ni kwanza kuacha akili yangu itulie kabisa ndio niamue niziwekeze wapi ili zinikwamue kimaisha”Alisema

“Nina mawazo kadhaa ya biashara ambayo nimekuwa nikiyawaza kama njia ya kutafuta namna ya kujikwamua kimaisha hivyo hizi pesa nitazielekeza huko ila baada ya akili yangu kwanza kutulia kutoka katika hali ya furaha niliyonayo sasa.”Aliongeza

Mshindi huyo ametumia pia fursa hiyo kuwashauri watanzania kutumia huduma ya M-PESA kwa kuwa mbali na kwamba imerahisisha maisha katika utumaji na upokeaji fedha mijini na vijijini bado wanaweza kuwa katika nafasi ya kushinda kama yeye

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza amesema promosheni hiyo imelenga kuwawezesha wateja wa M-PESA kubadili masiha kutokana na wanavyotumia huduma hiyo.

“Promosheni hii tulizindua mwezi uliopita tukilenga kuwawezesha wateja wetu kujishindia zawadi za fedha taslimu, kiasi cha Shilingi Milioni 480 kinashindaniwa ambapo hadi sasa wateja zaidi ya 4,000 wameshajinyakulia zaidi ya Shilingi Milioni 120” Alisema Bw. Rene

Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom wakishuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo. Katikati ni Ofisa Mkuu wa M-PESA Dylan Lenox. Jumla ya shilingi milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea ambayo inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 pindi mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.

No comments:

Post a Comment