Tuesday, March 27, 2012

BODI YA WADHAMINI YA HOSPITALI YA TAIFA YA ZINDULIWA.

Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. (MNH) Profesa Joseph Kuzilwa, akiwa katika picha baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Hadji Hussein Mponda kuzindua jana. Bodi hiyo ni ya Nne tangu kuanzishwa kwa Hospitali Taifa ya Muhimbili iliyojengwa Mwaka 1956 ikiwa na majengo matano na uwezo wa kuhudumia wagonjwa 10000 tu kwa ajiri ya mkoa wa Dar es Salaam,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda (katikati) waliokaa akiwa katika picha ya Pamoja na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuzindua Bodi hiyo jana katika hafla fupi iliyofanyika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akisisitiza jambo wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya Nne ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, wapili kutoka kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu Dkt.Donan Mmbando , Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Joseph Kuzilwa na Mkurugenzi wa Hositali ya Taifa ya Muhimbili Dkt.Merina Njelekela.

No comments:

Post a Comment