Wednesday, March 28, 2012

KAMPUNI YA VODACOM TANZANIA KUPITIA MRADI WAKE WA MWEI WAWANUFAISHA AKINA MAMA WAJASIRIA MALI WA MLANDIZI.

Waratibu wa mradi wa MWEI uliopo chini ya Kampuni ya Vodacom Tanzania. (kushoto) Mbaga Ally na Emmanualey Mgongo ,wakihakiki majina ya akina mama wajasiria mali toka vikundi mbalimbali wa kijiji cha Kilangalanga cha Mlandizi mkoa wa Pwani.Jumla ya akina mama 425 wamefaidika na mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 30.usiokuwa na liba yoyote.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, akifafanua jambo kuhusiana na mikopo ya MWEI kwa akina mama wajasiria mali toka vikundi mbalimbali katika kijiji cha Kilangalanga, Mlandizi mkoa wa Pwani. Jumla ya akina mama 425 wamenufaidika na mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 30.
Akina mama toka vikundi mbalimbali vya wajasiria mali toka katika kijiji cha Kalangalanga Mlandizi, wakifurahia kupata mkopo kutoka katika kampuni ya Vodacom Tanzania, kupitia kitengo chake cha MWEI. Jumla ya akina mama 425 wamenufaika na mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 30, kwa ajili ya kuendeleza bishara zao ndogondogo pasipo na liba yoyote.
Diwani wa Kata ya Janga, Fedilia Simba ,akimsisitizia jambo Meneja Mradi wa MWEI Mwamvua Mlangwa, wa Kampuni ya Vodacom, wakati wa hafla fupi ya kutoa mikopo kwa akina mama wajasiria mali wa vikundi mbalimbali vya kijiji cha Kilangalanga Mlandizi mkoa wa Pwani, Jumla ya akina mama 425. wamenufaika na mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 30 ambao hazitakuwa na liba yoyote wakati wa marejesho.

No comments:

Post a Comment