Wednesday, March 28, 2012

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA KUIMALISHA MKATABA WA BIMA YA AFYA.


Na Mwandishi wetu.

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) upo kwenye mchakato wa kukamilisha mkataba mpya wa huduma ya afya baina yao na hospitali Agakhan .

Awali mkataba wa kutoa huduma za matibabu kwa wanachama ambao wagonjwa wapya wanaotumia bima ya afya ulisitishwa tangu mwezi Februari mwaka huu.

Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Nsachris Mwamwaja alisema kuwa huduma hiyo inatarajia kuanza wakati wowote baada ya kukamilika kwa mkataba huo.

Alisema kuwa baada ya kukamilika kwa mkataba huo na mchakato wa hutoaji wa huduma za kawaida zitaendelea kama kawaida.

Mwamwaja alisema kuwa utoaji wa huduma zitategemea na makubaliano baina ya hospitali pamoja na NHIF.

Kwa upande Mkurugenzi wa Madawa Hospitali hiyo Dk. Jaffer Dharesee alikiri kuwepo kwa usitishwaji wa huduma kwa wanachama wa NHIF .

Alisema kuwa ingawa hakuweza kueleza kwa undani sababu ni ni ya kusitisha kwa huduma hiyo licha ya kubainisha sababu moja ikiwemo ya kuisha kwa mkataba baina yao na NIHF.

"Mkataba baina yetu na NHIF uliisha tangu mwezi wa Mei mwaka jana lakini tunaendelea kutoa huduma kwa magonjwa saba ikiwa ni pamoja na wale wagonjwa waliopewa ahadi kwa ajili ya upasuaji, ICU wanaendelea kupata huduma ila wale wanaotembea hawapati huduma ," alisema Dharesee

Akizungumzia kuhusu zoezi la ukaguzi wa hospitali , vituo vya afya na zahanati za Umma na binafsi alisema kuwa limeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Alisema kuwa wale waliobainika wana upungufu wamejirekebisha ikiwa na wengine ambao hawakuhusika katika zoezi hilo wamefanyia mapungufu yao.

"Kwa kweli zoezi hili ni mwendelezo hivyo limesaidia sana kwani wale waliobainika wana mapungufu wameweza kuyafanyia kazi na hata wale ambao hakuguswa na zoezi hilo waliweza kufanyia kazi mapungufu yao," alisema Mwamwaja.

Msemaji huyo alisema kuwa zoezi hilo linaendelea kufanyika katika Halmashauri na mikoa ikiwa lengo ni kuhakikisha huduma za afya nchini zinaimarishwa na kutolewa kwa bora.

No comments:

Post a Comment