Wednesday, March 28, 2012

RAIS KIKWETE AFUNGUA WARSHA YA MIKAKATI YA KUONDOA UMASKINI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe, Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Saidi Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka hoteli ya White Sands Hotel alikofungua warsha ya siku mbili ya Utafiti.

Rais DktJakaya Mrisho Kikwete akiongea na Profesa Ibrahim Lipumba baada ya picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya siku mbili ya utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini.

Profesa. Do Duc Dinh toka Vietnam akitoa mada ya jinsi nchi yake ilivyofanikiwa kuondoa umaskini katika warsha ya siku mbili ya utafiti wa mageuzi ya kuondoa umaskini nchini.PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment