Tovuti yako uipendayo inakupa huduma ya kujivinjari bure kutoka Uhuruone
Muhidini Issa Michuzi akishikiriana na Uhuruone wanawapatia wakazi wote wa
Akikaririwa katika mahojiano ndugu Issa Michuzi alisema hivi, “Ni mapinduzi ya kweli ambapo Watanzania wanachukua hatua katika kuleta taarifa mbalimbali kwa wananchi katika viwango nafuu. Ninaamini hii itaongeza mawasiliano kwa watu wetu na ni ndoto yangu kwamba tovuti ya Michuzi itakua huru kufika kwa Watanzania wote hivi karibuni”.
Akiwa ofisini Bwana Rajabu Katunda alisema, “Uhuruone imejikita katika kutoa huduma kwa jamii na tumegundua kwamba taarifa za kijamii zinatakiwa kuwafikia wanajamii kwa urahisi. Tovuti nyingi zinatembelewa na Watanzania waliopo nchi za nje kuliko wananchi waliopo nchini na hii siyo haki. Kama nina uwezo kupata taarifa kwenye tovuti ya Michuzi ni jukumu letu
Kwa pamoja Bwana Michuzi na Katunda wamesema huu ni mwanzo tu na wanaamini kwamba hili wazo litafuatwa na wengine. Kwa msisitizo Bwana Michuzi aliongea “Lazima tuonyeshe mfano kwa vitendo sio maneno tu. Tumechukua hatua ya kwanza katika kufanikisha ndoto, wengine wanatakiwa kujiunga kwenye mapinduzi haya na kufanikisha”
Kutembelea tovuti ya Michuzi bila gharama washa Wifi kwenye Ipad, Tablet, Simu au Laptop. Tafuta Michuzi blog Wifi, Unganisha ,fungua browser yako uipendayo mfano Chrome, Internet Explorer, Safari au Firefox na nenda kwa Issa Michuzi.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment