Tuesday, April 10, 2012

MAZISHI YA STEVEN KANUMBA YAWA YA HISTORIA TANZANIA UMATI WA WATU WAFURIKA ZOEZI LA KUAGA MWILI WAKE LASHINDIKANA.

Umati wa watu wakiwa katika halakati za kwenda katika mazishi ya Kanumba katika makaburi ya Kinondoni eneo la barabara ya Kinondoni.
Hatuamini hadi tujionee wenyewe baadhi ya waombolezaji wakiwa wamepanda juu ya mti ili waweze kuona mazishi yalivyokuwa yakiendelea katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Askari wa Usalama kitengo cha farasi akijaribu kumwelekeza mmoja wa waombolezaji waliofika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wengi wa wananchi hawakufanikiwa kuona mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho kutokana na umati wa watu kuwa wengi,ilishindikana kuaga.
Askari polisi wakiweka alama ya kuziwia watu wasiingie eneo la mazishi lakini ilishindikana.
Kamanda wa Kanda maalumu Sulemani Kova akiwatangazia watu kuwa wavumilivu na kutii sheria ili mazishi yaweze kwenda sawia.

No comments:

Post a Comment