Gazeti
la Tanzania Daima la jana Jumapili Aprili 22, 2012 lina habari katika ukurasa wake wa mbele yenye
kichwa cha habari ‘JK alinda Mawaziri’,
inayodai kumekuwa na mazungumzo
baina ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kuhusu
hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.
Habari
hiyo imedai kuwa Mhe. Pinda anataka
mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini,
lakini, imeendelea kudai habari hiyo, “Rais
Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hili
ni la upepo tu, liachwe litapita”.
Tunachukua
nafasi hii kuweka bayana kwamba habari katika hilo hazeti la Tanzania Daima
Jumapili si za kweli, bali ni za uzushi na upotoshaji mkubwa.
Mheshimiwa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini
Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala kufanya mazungumzo
na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.
Hivi
sasa Mhe. Rais anasubiri kupata taarifa rasmi
kutoka Bungeni Dodoma.
Mhe
Rais anawasihi wananchi wasiamini habari hizo za upotoshaji zilizomo kwenye
gazeti hilo la Tanzania Daima Jumapili.
Pia
ametoa rai kwa wanahabari wasitoke nje ya mstari wa weledi katika kutekeleza
kazi zao ili kuendelea kulinda heshima zao binafsi, vyombo wanavyofanyia kazi
pamoja na taaluma yenyewe.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment