Wednesday, May 23, 2012

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAWASILIANO ,SAYANSI NA TEKNOLOJIA JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA KAMPUNI YA VODACOM TANZANIA.


  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba  akizungumza na  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza.wakati alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni hiyo iliyopo Mliman City jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (kulia) wakibadilishana uzoefu kabla ya Naibu Waziri kufanya mazungumzo na watendaji wakuu wa Vodacom Tanzania  wakati alipofanya ziara ya utambulisho katika Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam.
  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba akikaribishwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza, wakati alipotembelea Makao Makuu ya Vodacom Tanzania jijini Dar es salaam, na kufanya mazungumzo na viongozi wa kuu wa Vodacom.


 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi an Teknolojia January Makamba akikaribishwa Makao Makuu ya Vodacom Tanzania na Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Mauzo kwa Wateja Wakubwa waVodacom Tanzania Mwamvita Makamba. wakati alipofanya ziara ya kutembelea kampuni ya  Vodacom Tanzania na kukutana na Uongozi wa kampuni hiyo. 
KARIBU SANA HAPA KWETU JISIKIE UPO NYUMBANI,  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba akilakiwa na Mkuu wa Mahusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Joseline Kamuhanda. Makamba alitembelea makao makuu ya Vodacom katika ziara ya kujifunza shughuli za kampuni hiyo. Katikati ni Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim.

No comments:

Post a Comment