Wednesday, June 6, 2012

MANJI ATIMULIWA KATIKA JENGO LAKE LA QUALITY PLAZZA.





share

Yusuf ManjiSAKATA  la Mfanyabiashara Yusuf Manji na mifuko ya hifadhi ya jamii limeendelea na sasa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), umemtaka mfanyabiashara huyo kuhama mara moja katika jengo la Quality Plaza ambalo aliuuzia mfuko huo katika mazingira tata.
Manji anadaiwa na PSPF karibu Sh bilioni 5, ambazo ni malimbikizo ya kodi ya pango.
Kwa muda mrefu sasa Manji amekua akitajwa kufanya biashara zenye utata na mifuko ya hifadhi ya jamii na alifanikiwa kuiuzia PSPF jengo la Quality Plaza na Mufuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuizua maghala kwa shilingi bilioni 46, ambayo aliyajenga kwa mkopo wa Sh bilioni 9 kutoka mfuko huo.
Habari za uhakika kutoka serikalini zinaeleza kwamba, uamuzi huo wa PSPF umefikiwa Ijumaa ya Aprili 1, 2011 baada ya mfuko huo kubanwa na Wabunge wa Kamati Hesabu za Mashirika ya Umma  (POAC), inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe .
Katika barua ya PSPF  kwenda kwa kampuni ya Image Properties & Estate inayosimamia uendeshaji wa Quality Plaza, mfuko huo umeitaka kampuni ya Quality Group Limited kuondoka mara moja katika jengo hilo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Hivi karibuni, Quality Group Limited iliiomba Mahakama kuzuia kuondolewa kwao katika jengo hilo, maombi ambayo muda wake ulishakwisha lakini PSPF wakawa wanachelewa kuchukua hatua wakati taasisi hiyo ilikua na hali mbaya ya kifedha kiasi cha serikali kuombwa na POAC kulinusuru kwa kuwekeza zaidi.
“Unaelekezwa kuitimua haraka Quality Group Limited kwa kushindwa kutimiza masharti ya mkataba wa pango,” inaeleza sehemu ya barua hiyo ya Aprili 1, 2011 iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi  Adamu Mayingu, kwenda kwa Image Properties & Estate.
Manji afukuzwa Quality Plaza
Jengo hilo liko kitalu namba 182/2 barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam ni mali ya PSPF alipanga baada ya kuliuza lakini akawa halipi kodi.
Katika maelezo ya wakili wa PSPF, Benitho Mandele, ambayo iliwasilishwa mahakamani iilieleza kwamba Manji anadaiwa kodi ya kuanzia Aprili, 2009 hadi Desemba 2010, hivyo jumla ya deni lote ni dola 2,335,189.06 za Marekani, wakati shauri hilo lilipowasilishwa mahakamani na sasa limefikia Sh bilioni 5.
Makampuni mengine ya Manji yaliyomo katika jengo hilo ni pamoja na kampuni aliyoichukua kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mazingira tata ya Gaming Management Limited, Quality Ligistics Co. Limited, International Transit Ivestment Limited na Q-Consult Limited.
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/5 (0 votes cast)

No comments:

Post a Comment