Wednesday, June 6, 2012

SIMBA KUPELEKA KOMBE KANDA YA ZIWA

 Mwenyekiti wa klabu ya Simba Aden Rage akiongea na waandishi wa Habali leo katika ukumbi wa mikutano wa TBL kuhusiana na ziara ya timu ya Simba itakayokwenda  kusherehekea Ubingwa  wa Kombe katika Kanda ya Ziwa ambapo itacheza mechi za kirafiki katika Mkoa wa Shinyaga itacheza na Toto Afrika  mnamo tarehe 16 mwezi huu na kufuatiwa na Mkoa wa Mwanza, tarehe 17,ziara hiyo imeratibiwa na TBL ambayo ndiyo mdhamini mkuu kupitia bia yake ya Kilimanjaro Prrmium Lager.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lage George Kavishe kulia akimsikiliza Mwenyekiti wa Timu ya Simba Adan Rage wakati alipokuwa akiongelea ziara ya timy yake itakayofanyika katika mikoa ya kanda ya ziwa ya Shinyanga na Mwanza ikiwa nikuwapa wanachama na mashabiki wa simba kufarahia mafanikio ya timu yao na kujionea jinsi walivyofanya usajili mwaka huu.
Mwenyekiti wa Klabu ya simba Adan Rage akiongea kuhusiana na safari ya simba kwenda kanda ya ziwa wakati aliokutana na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager George Kavishe.

No comments:

Post a Comment