Sunday, June 10, 2012

WHITEDENT WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA FRIENDS OF DON BOSCO.

 Wanafunzi wa Shule ya msingi Mgulani jijini Dar es Salaam, wakipanga zawadi zao za mipira,dawa ya meno na vifaa vingine vingi wakati walipofika katika kituo cha kule watoto waishio katika mazingira magumu wanao lelewa katika kituo cha Friends of Don Bosco Kimara Suka jijini Dar es Salaam.  Kampuni ya Chemi& Cotex  Ltd  ambayondiyo watengenezaji wa dawa ya Whitedent ndiyo iliyotoa vifaa hivyo
 WandeOkoth akiongea na watoto wanaolelewa katika kituo cha Don Bosco kilichopo Kimara Suka jijini Dar es Salaam, wakati  kampuni yake ya Chemi & Cotex waliopokwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo dawa za meno za Whitedent na vitu vingine ,
 Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Don Bosco akiwapokea wageni wake huku akiwaamemeba zawadi.
 Watoto wakipata msosi walioandaliwa na WHITEDENT
 Watoto wakipata msosi walioandaliwa na WHITEDENT.
 Mwanzilishi wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Don Bosco  Evans Tegete akimkaribisha ...... wakati waliopfika katika kituo hicho kuwakilisha msaada wa dawa za meno za Whitedent na vitu mbalimbali.
  Mungu awabariki sana Whitedent.
 Baadhi ya watoto wanaolelewa  katika kituo cha Donbosco wakiwa na zawadi ya mpira baada ya kupewa msaada.
 Aksanteni sana Whitedent tutaweza kupiga mswaki meno yetu, watoto wanaolelewa katika kituo cha DonBosco wakiwa wamenyenyua dawa walizopewa msaada na Kampuni ya Chemi&Cotex  Industry Ltd  ya jijini Dar es Salaam.
  Watoto wanao lelewa katika kito cha Don bosco wakipewa msaada wa Dawa za Meno na watoto wenzao wa shule ya msingi mgulani.
 Mabalozi wa dawa ya meno ya Whitedent ,Zuwena Omari,Aisha Abdallah wakiwakabidhi msaada wa dawa za meno watoto wanaishi na kulelewa katika kituo cha Friends of Don Bosco kilichopo Kimara Suka jijini Dar es Salaam.
Mtoto aliyefahamika kwa jina la Yusuph (katikati) akiwaonyesha wenzake moja ya zawadi aliyopewa na  wanafunzi wa Shule ya Mgulani jijini Dar es Salaam, Kampuni ya Chemi& Cotex Ltd, inayojihusisha na utengenezaji wa Dawa za Meno ya Whitedent kupitia wanafunzi hao walitua ,vitu mbalimbali ikiwemo mipira ya kuchezea na dawa za meno kwa watoto waishio katika mazingira magumu wanaolelewa katika kituo cha Friends of DonBosco.

No comments:

Post a Comment