Tuesday, August 28, 2012

BAADA YA KUHITIMU MAFUNZO AKABIDHIWA ZAWADI TV.

Bibi yake Josephine Ndauka akimkabidhi zawadi ya TV David Njombe.

KUA UYAONE BABA. David Njombe anayetegemea kufunga ndoa siku ya Jumamosi hii katika kanisa Katoliki Mwenege jijini Dar es Salaam, Jumapili iliyopita ilikuwa ya aina yake kwake baada ya kukalishwa chumbani kwa siku nzima akipewa mafunzo ya kuweza kuisha na mke pindi atakapo oa  ikiwa ni njia moja wapo ya kumkumbusha maadili, mila na desturi za kutunza familia . 

Shuguli hiyo iliyoongozwa na mmoja wa wachamungu alikuwa ya mafanikia baada ya mkufunzi huyo kugundua kuwa kijana huyo aliweza kuuliza maswali mabnlimbali yenye mrengo wa kiimani, jioni ya siku hiyo ndugu jamaa wa karibu na familia hiyo walifanya kitafrija kidogo cha kumfunda Bag Part ambapo akina mama walioongozwa na bibi yake waliweza kumweleza njisi ya kuishi na mke na zaidi awe mcha mungu kwani Mungu ndiye pekee kimbilio la kila kitu, 

Wamama hao wakiongozwa na mama yake mlezi waliweza kumzawadia zawadi ya  TV ya kisasa  yenye thamni ya shilingi Laki Tano

Harusi ya David itafanyika siku ya Jumamosi katika Kanisa Katoliki la Mwenge na kufuatia na sherehe ambayo itafanyika katika ukumbi wa Delus Sinza jijini Dar es Salam.
Hayawi hayawi yamekuwa Bwana harusi Joshua Madeleka akiwa na Mkewe katika pozi la picha baada ya kufunga ndoa yao hivi karibuni katika kanisa la Morovian Ukonga na kufuatiwa na sherehe kubwa ilityofanyika Landmark Hotel jijini Dar es Salaa.

No comments:

Post a Comment