Friday, August 10, 2012

MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA JAJI JOSEPH WARIOBA ALIVYOKUTANA NA WANANDISHI WA HABARI KUZUNGUMZIA MAENDELEO YA ZOEZI LA KUKUSANYA MAONI KWA WANANCHI .

 Mwandishi wa EAST AFRICA TV, Noha akiuliza swali.
 Waandishi kazini mwandishi wa TBC Elisha Elia akiongoza mashambulizi.
 Waandishi wa Habari  wakiwa kazini wakati wa Mkutano na Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu maoni ya Katiba.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake kuhusiana na Tathmini ya kazi ya kukusanya maoni katika mikoa minane iliyopangwa kufikia katika hatua ya kwanza.ambayo ilikuwa ni Pwani,Daodoma,Kagera,Shinyanga,Tanga,Kusini Unguja,Pemba, ambapo alisema kuwa mikutano katika mikoa hiyo ilianza Julai 2 hadi Julai 30 mwaka huu.

Ambapo alibainisha kuwa jumla ya mikutano iliyofanyika katika mikoa hiyo ilikuwa ni 386.kati ya mikutano hiyom tume lifanya mikutano 8 maalum,idadi ya watu waliohudhulia mikutano hiyo ilikuwa 188,679 ikiwa ni wastani wa 489 waliofika kila mkutano.Jumla ya wananchi waliotoa maoni ni 17,440 kwa njia ya kuzungumza kwenye mikutano,Jumla ya wananchi 29,180 walitoa maoni kwa njia ya maandishi,

Warioba alisema kuwa awamu ya pili ya ukusanyaji wa maoni kuhusu katiba mpya katika mikoa ya Mbeya,Kigoma,Morogoro,Lindi,Ruvuma,Katavi,na Mwanza itaanza Agosti 27 mwaka huu na kumalizika Septembe 28 ,2012.

No comments:

Post a Comment