Friday, September 21, 2012

BENKI YA KCB TANZANIA YATOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI KWA HOSPITALI ZA TEMEKE NA BUGURUNI VYOTE VIKIWA NA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 17,152,000.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, DR.Amani Malima akitoa neon la shukrani kwa wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania kwa kuwakabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya Hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni 11.252.000.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Buguruni jijini Dar es Salaam,DR.Hawa Lesso akiushukuru uongozi na wafanyakazi wa benki ya KCB Tanzania kwa kuwakabidhi msaada wa Mashine ya Joto ya watoto njiti waliozaliwa kabla ya wakati wao 1 (Baby Warmer Mashine) yenye thamani ya shilingi Milioni 5.9.katika hafla iliyofanyika katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa benki ya KCB Tanzania wakiwa katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali katika  Hospitali  ya Temeke na Buguruni zote za jijini Dar es Salaam, vifaa vilivyotolewa msaada na benk hiyo  ni pamoja na Mashine ya  joto ya ya watoto njiti, sare za wauguzi 10,Mashine ya kusaidia kupumulia wagonjwa (SET OF OXYGEN FLOW METER ) vyenye thamani ya shilingi milioni 17,152.000.


Mkurugenzi wa Bodi wa Benki ya KCB Tanzania Mama Zuhura Muro akihutubia wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vya hospitali ya Temeke na Buguruni zote za jijini Dar es Salaam,vyenye thamani ya shilingi Milioni 17,152. Hafla hiyo ilifanyika katika Hositali ya Temeke.



 Mkurugenzi wa Bodi wa Benki ya KCB Tanzania Mama Zuhura Muro,(kulia) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, DR.Amani Malima,mashine ya kumsaidia mgonjwa kupumulia wakati wa hafla ya kukabidhiwa vitu mbalimbali kwa ajiri ya Hospitali ya Temeke na Buguruni vyenye thamani ya shilingi Milioni 17.152.000.(katikati) Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Temeke James Magoti.
Mkurugenzi wa Bodi wa Benki ya KCB Tanzania Mama Zuhura Muro,(kulia) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Buguruni jijini Dar es Salaam, DR.Hawa Lesso msaada wa mashini ya joto inayosaidia kutunzia motto aliyezaliwa kabla ya wakati wake (NJITI)  katika hafla iliyofanyika Hospitali ya Temeke, Benki ya KCB ilitoa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 17,152,000. Wanaoshuhudia ni wauguzi wa ahaospitali ya Buguruni waliofika kupokea msaada huo.


Wauguzi wa hospitali ya temeke wakifurahia msaada wa mashine ya joto inayosaidia watoto wachanga waliozaliwa kabla ya mda wake Njiti, baada ya kukabidhiwa msaada na benki ya KCB.

 Wauguzi wa Hospitali ya Temeke na Buguruni wakiwa katika hafla hiyo
Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa benki ya KCB Christina Manyenye akizungumzia juu ya huduma zitolewazo na benki hiyo wakati wa hafla ya kukabidh vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 17,152,000.

No comments:

Post a Comment