KAMATI YATANGAZA MCHAKATO WA UCHAGUZI TWFA
Kamati
ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA)
kimetangaza mchakato wa uchaguzi wa chama hicho ambao unaanza kesho
(Septemba 23 mwaka huu).
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ombeni Zavala, mchakato utaanza
kesho ambapo fomu zitatolewa ofisi ya TWFA ambayo iko Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10
jioni.
Mwisho
wa kuchukua na kurudisha fomu ni Septemba 27 mwaka huu. Nafasi
zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Mhazini, Mjumbe
wa Mkutano wa TFF, na wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji.
No comments:
Post a Comment