Release No.
146
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Septemba 16,
2012
SERENGETI BOYS
YAENDELEA KUJINOA
Timu ya Taifa
ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) inaendelea vizuri na
kambi ya mazoezi katika mikoa ya Mbeya na Njombe ambapo leo jioni (Septemba 16
mwaka huu) itacheza mechi ya kirafiki mjini Makambako na timu ya
Manispaa.
Serengeti Boys
ambayo iko chini ya Kocha Jakob Michelsen na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo
imeshacheza mechi nne mkoani Mbeya. Imecheza mechi hizo dhidi ya Tanzania
Prisons, Mbozi United, Mbeya City na Kombaini ya Kyela na kupoteza moja
tu.
Baada ya mechi
ya leo, kesho (Septemba 17 mwaka huu) itacheza mechi ya mwisho mkoani Njombe
dhidi ya Kombaini ya Makambako na kurejea Dar es Salaam siku inayofuata kwa
ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya mechi dhidi ya
Misri.
Mechi hiyo ya
kwanza ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa vijana
zitakazofanyika Machi mwakani nchini Morocco itachezwa Oktoba 13 mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
MECHI YA
SIMBA, LYON YAINGIZA MIL 67/-
Mechi ya Ligi
Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na African Lyon
iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 67,793,000.
Washabiki
11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh.
5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 14,603,263.47
wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh.
10,341,305.08.
Mgawo mwingine
umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh.
114,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, et iti.sh. 3,175,000, vishina kwenye
tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh.
400,000 na Wachina (stadium technical support) sh.
2,000,000.
Umeme sh.
300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh.
4,867,754.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,920,652.69,
uwanja sh. 4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,947,101.86, gharama za mchezo sh. 4,867,754.49.
Nayo mechi ya
ligi hiyo kati ya Tanzania Prisons na Yanga iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka
huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh.
50,435,000.
112 WASHUHUDIA
MECHI YA JKT RUVU v RUVU SHOOTING
Watazamaji 112
ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu
na Ruvu Shooting iliyofanyika jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Azam
Complex, Dar es Salaam.
Mapato
yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh.
10,000 ni 340,000. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 29,465.87,
asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 51,864.40, maandalizi ya
uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 89,916.
Kamati ya Ligi
sh. 9,821.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,893.17, Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,928.78, gharama za mchezo sh.
9,821.95 na uwanja sh. 9,821.95.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment