Friday, October 19, 2012

MKUTANO WA KURASIMISHA MATOKEO YA UTAFITI ULIOFANYA MIONGONI MWA WANAWAKE WANAOFANYA BIASHARA YA NGONO DAR ES SALAAM UKUMBI WA Dar es Salaam


 Mkurugenzi Msaidizi wa Afya na Usafi wa Mazingira Eilias Chinamo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani Juu ya Ripoti ya Utafiti Uliofanyika Dar es Salaam,miongoni mwa Wanawake wanaofanya biashara ya Ngono  ambapo kwa hapa jijini ni 7,500.katikati ni Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Kuratibu Mipango ya Ukimwi na Kushoto ni Mkuu wa Ufuatiliaji wa Magonjwa CDC DR. Marry Kibona.

            Remarks by U.S. Centers for Disease Control and Prevention (CDC)
Epidemiology/Survelliance Team Lead, Dr. Mary Kibona
Kirimjee Hall, Dar es Salaam
October 19, 2012


Kaimu Mganga Mkuu  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donnan Mmbando

Mwenyekiti, tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI

Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kupambana na UKIMWI

Mganga Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam

Mratibu wa UKIMWI wa Mkoa wa Dar es Salaam na Manispaa

Wawakilishi wa taasisi za kitaifa na kimataifa

Wawakilishi wa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Ndugu wana habari

Wageni Waalikwa

Waheshimiwa, mabibi na mabwana,


Habari za asubuhi?


Kwa niaba Shirika la Kimarekani la Kudhibiti Maradhi na Kinga (CDC) na Serikali ya Watu wa Marekani, ninafurahi kuwakaribisha.  Ninayo furaha kuungana nanyi katika siku ya kuwasilisha ripoti ya utafiti uliofanywa miongoni mwa wanawake wanaofanya biashara ya ngono hapa Dar es Salaam mwaka 2010.
Katika mwaka 2003, Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI (PEPFAR) ulianzishwa.  Serikali za Marekani na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ziliunganisha nguvu kupambana na mlipuko wa UKIMWI. 

Tangu wakati huo, kupitia jitihada za pamoja zimekuwa zikifanywa, na tumeweza kusonga mbele ambapo Watanzania wengi wamefaidika.  Ni ukweli usiyofichika kwamba Watanzania wengi wanapata matibabu na huduma za afya ambavyo vimepunguza vifo.  Tunaweza na kustahili kujivunia kushirikiana wa nchi mbili hizi.  Hii inaonyesha tuna lengo moja.

Hata hivyo tunaelewa kwamba bado kuna kazi kubwa na watu wengi wanaohitaji kusaidiwa, bado hawajapata huduma hizi.  Kwa hiyo, sasa tumeanza kutumia uzoefu uliopo na tunabadilisha mikakati ili kuwa na ufanisi na kuwasaidia wengi.  Kwa mudu wote huu tumejifunza mambo mengi na sasa tunalenga zaidi kumaliza mlipuko huu.

Kutokana na kwamba mpango wetu wa UKIMWI umekuwa na PEPFAR imebadilika kutoka mpango wa dharura na kuwa mpango ndelevu wa nchi hii, tumetambua kwamba baadhi ya mipango itatakiwa kuwa na mikakati zaidi na mwelekeo thabiti. 

Tunaelewa kwamba ili kufikia lengo letu la Tanzania bila UKIMWI, ni lazima kukumbuka makundi maalum ya watu walio katika mazingira hatarishi ya kupata maambukizi ya VVU, yaani “key populations.”

Kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton alivyosema hivi karibuni katika mkutano wa kimataifa wa UKIMWI Duniani 2012, “Tukitaka kuokoa maisha, tunatakiwa kwenda haraka mahali VVU vilipo, huku tukiongozwa na vigezo vya kisayansi.”

Shirika la Kimarekani la Kudhibiti Maradhi na Kinga (CDC), litajitahidi kuwafikia watu hawa walio katika mazingira hatarishi ya kupata maambukizi ya VVU na kuelewa mchango wao katika mlipuko wa UKIMWI. Wakati wote tumejivunia kuzisaidia tafiti na afua mbalimbali zinazoshirikisha makundi haya. Kwa mfano, tumeshasaidia sana kuanzishwa kwa mradi wa kuwatibu watu wanaotumia dawa za kulevya.  Tunayo furaha kwa kuwa mwendelezo wa juhudi hizo sasa umewafikia wanawake wanaofanya biashara ya ngono. 

Utafiti kama huu tunaouadhimisha leo ni muafaka na nyenzo muhimu tunazohitaji kuwa nazo na kutekeleza afua zenye matokeo muhimu kwa makundi haya.  Utafiti huu ulioshirikisha zaidi ya wanawake 500 wanaofanya biashara ya ngono na unatoa taarifa muhimu inayotakiwa ya mlipoko wa UKIMWI hapa Dar es Salaam.
Kutokana na dhamira iliyoonyeshwa na PEPFAR kupitia CDC kwa kushirikiana na serikali za nchi nyingine tafiti kama hizi zimeshafanywa huko Msumbiji, Uganda, Kenya, Namibia na Zanzibar.  Na sasa ni fahari kuongeza Tanzania katika orodha hii.  Matokeo haya yote yatatumika kuandaa mikakati ya kukabiliana na UKIMWI.
 Tunatambua kwamba washikadau mbalimbali walishiriki kwa njia moja au nyingine kufanikisha utafiti huu. 
 Ninachakua nafasi hii kuwashukuru Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi za Jamii Muhimbili (MUHAS) na Chuo Kikuu cha California San Francisco (UCSF) kwa kutoa mshauri wa kitaalum.
 Nanipasa kumshukuru mgeni rasmi na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Mpango wa Taifa wa Kupambana na UKIMWI (NACP) na Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na Ubora (NHLTC)  kwa kuongoza juhudi hizi. 

Itakuwa ni utovu wa nidhamu kutowashukuru wanawake walioshiriki katika utafiti huu.  Bila hawa ripoti hii isingepata taarifa/takwimu stahili. 

Mwisho, kwa niaba Shirika la Kimarekani la Kudhibiti Maradhi na Kinga (CDC) na Serikali ya Watu wa Marekani, napenda kutumia nafasi hii kurejea ahadi yetu ya mapambano dhidi ya UKIMWI na kuboresha afya ya Watanzania wote, ikiwa pamoja na watu walio katika mazingira hatarishi ya kupata maambukizi ya VVU.  Hatuwezi kusahau hawa. 
 Ni matarajio yetu kuona faida za utafiti huu zikitumika

No comments:

Post a Comment