WAKATI Uchaguzi wa Umoja
wa Wanawake Tanzania (UWT) umemalizika juzi, huku ukidaiwa kugubikwa na
ubabe na rushwa, Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umejitapa kwamba,
utahakikisha vitendo hivyo havitokei katika uchaguzi wake mkuu
utakaofanyika kesho mjini Dodoma.
UVCCM imeapa kwamba mgombea au hata mpambe
atakayebainika kujihusisha na kampeni zilizo nje ya utaratibu na kanuni
za UVCCM au kujihusisha na vitendo vya rushwa atashughulikiwa mara moja
ikiwemo kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa,
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM,Martine Shigela alisema, wameweka
mtandao mpana wa kutosha kukabiliana na aina yoyote ya ukiukwaji wa
tararibu, kanuni na sheria za uchaguzi wa UVCCM.
"Sisi hatuwezi kuzungumzia hayo mnayosema,
yamejitokeza kwenye uchaguzi wa UWT,lakini kwa upande wetu
tunawahakikishieni kwamba tutamkabili vilivyo tena bila mzaha,mgombea au
mpambe yeyote atakayejaribu kutumia mbinu chafu za kampeni ikiwemo
kutoa rushwa", alisema Shigela.
Shigela alisema, taratibu za mkutano mkuu
utakaoambatana na uchaguzi huo, zimekamilika na utafanyika kwenye ukumbi
wa Mwalimu Nyerere, uliopo Chuo Cha Mipango ambako ndiko ulikofanyika
pia ule wa UWT.
Alisema, mkutano unaanza kesho, Oktoba 23, na
utafunguliwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete."Hadi sasa
maandalizi yamekamilika, leo Oktoba 22, tunakazi kupokea wageni
mbalimbali kutoka maeneo kadhaa wakiwemo wa kutoka nchi za nje amabao
watahudhuria mkutano wetu. alisema Shigela.
Katika nafasi ya Mwenyekiti wanachuana wagombea
watatu, Lulu Mushamu Abdallah, Sadifu Juma Khamis na Rashid Simai
Msaraka wakati katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Ally Salum Hapi,
Paul Christian Makonda Mboni Mohamed Mhita.
Nafasi zingine ni, Halmashauri Kuu ya Taifa Viti
sita (Bara) wagombea 40, Viti Vinne (Zanzibar) wagombea 22, Nafasi ya
Baraza Kuu la Vijana Taifa Viti vitano Bara wagombea 39 na viti vitano
Zanzibar wagombea 14, Uwakilishi Wazazi Taifa na Jumuia ya Wanawake
Tanzania (UWT) wagombea 16 kila nafasi.
No comments:
Post a Comment