Monday, October 1, 2012

OMMY DIMPOZ ATOA SABABU YA KUFANYA VIDEO NJE


Na blogs ya Habari Mseto.

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amesema aliamua kwenda kufanya video ya wimbo wake wa ‘Baadae’ nchini Afrika Kusini kutokana na usumbufu wa wamiliki wa sehemu husika ambayo amepanga kufanyia kazi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ommy alisema, Tanzania kuna sehemu nyingi za kufanyia kazi, lakini wamiliki wa sehemu husika huwa hawana imani na baadhi ya wasanii ambao wataomba kufanyia kazi sehemu hiyo.

“Nikielezea jinsi nilivopata shida kufanya video ya ‘Nai nai’, huwezi amini na kunawatu wengine walikuwa wananiruhusu kurekodi katika maeneo ambayo sio yakwao na hivyo kusababisha kufukuzwa kazi na mabosi wao,” alisema Ommy.

Akizungumzia kazi zake alisema, ‘Baadae’ ni muendelezo wa wimbo wake wa ‘Nai nai’ ambapo alikuwa anafikisha ujumbe kwa msichana ambae alikuwa anamsumbua kwa muda mrefu na baada ya kumkubali anamwambia waonane tena baadae.

Nai nai ni wimbo ambao ulimtambulisha msanii huyo na kumfanya aweze kuchukua tuzo mbili kwenye Kilimanjaro Music Award mwaka huu.

 Aliongeza kuwa, anajipanga kuachia ngoma yake mpya ambayo bado hajaipatia jina kutokana na ubora wa kazi hiyo, na anawaomba mashabiki na wadau wa kazi zake waendelee kumpa sapoti katika kazi zake.

No comments:

Post a Comment