Tuesday, October 9, 2012

USAFIRI JIJINI DAR.

 Abiria wakiwa   wamejazana katika basi linalalofanya safari   zake za Ubungo na Mbagara jijini Dar es Salaam,abiria wengi wamekuwa wakiibiwa kutokana na msongamano wa watu zaidi kulingana na uwezo wa gari lenyewe.
Mkuu wa kitengo cha huduma rejareja  za kibenki wa benki ya NBC Mmoloki Lesodu akibofya kitufe cha Komputa wakati kuchezesha droo ya washindi kumi wa shindano la Dabo Mshiki wako na NBC uliofanyika hivi karibuni  jijini Dar es Salaam,jumla ya washindi Kumi walipatikana. kutoka Kushoto ni Msimamizi kutoka bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania , Emmanuel Ndaki,Meneja Chapa na Matangazo wa NBC Aroen Kitomari na Mshauri wa Mahusiano wa benki hiyo Eddie Edward.
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akihutubia wakati wa sherehe ya uzinduzi wa DBC Commercial Bank  na Uhamasishaji wa ununuzi wa Hisa za haki uliofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo Poul Rupia. 

No comments:

Post a Comment