Congo
Brazzaville imewasili leo alfajiri (Novemba 15 mwaka huu) kwa ajili ya
mechi ya raundi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 dhidi ya Tanzania
(Serengeti Boys) itakayochezwa Jumapili.
Timu
hiyo imewasili kwa ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na msafara wa watu
30 wakiwemo wachezaji 18 ambapo imefikia kwenye hoteli ya Sapphire.
Mechi hiyo itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10
kamili jioni.
Serengeti
Boys inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa chini ya Kocha wake
Jackob Michelsen wakati Congo inafanya mazoezi leo jioni Uwanja wa
Karume, na kesho (Novemba 16 mwaka huu) asubuhi na jioni itafanya
mazoezi kwenye uwanja huo huo.
Timu
hiyo ambayo katika raundi ya pili iliitoa Zimbabwe itafanya mazoezi
yake ya mwisho Jumamosi jioni kwenye Uwanja wa Taifa. Viingilio kwenye
mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa VIP A, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP C ni
sh. 2,000 tu. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu ni
sh. 1,000 tu.
Makocha
wa timu zote mbili na manahodha wao watakutana na waandishi wa habari
Jumamosi saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kuzungumzia maandalizi yao kwa ajili ya mechi hiyo
kabambe.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF
No comments:
Post a Comment