Kumekuwepo
na malamiko kutoka kwa baadhi ya wadau wa mpira wa miguu kuhusu tarehe
ya uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Shirikisho linapenda kueleza kuwa suala hilo lilijadiliwa kwa kina
kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Novemba 3, 2012
kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa. Kikao kilimpa mwenyekiti
wa Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji kwa kushirikiana na
Sekretarieti jukumu la kushughulikia suala hilo. Tayari suala hilo
limeshashughulikiwa na ufafanuzi wote utatolewa na mwenyekiti wa Kamati
ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji katika mkutano na waandishi wa
habari siku ya Jumamosi ya Novemba 17, 2012 kuanzia saa 6:00.
Angetile Osiah
Katibu Mkuu TFF
No comments:
Post a Comment