NA BASHIR NKOROMO, GAIRO
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kukerwa kwake na matukio ya kejeli matusi na uvunjifu wa amani yanayoanza kushamiri bungeni
na kusema kuwa matukio hayo ni dhihaka ya hali ya juu inayofanywa na wabunge dhidi ya wananchi waliowachagua.
Hayo yalisemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati akizungumza kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa shule ya Msingi, Gairo mkoani
hapa, Aprili 18, 2013, ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana.
" Mambo haya yanayofanywa na wabunge kama
ilivyotokea jana (juzi), ni dhihaka inayofanywa na wabunge kwa wanancjhi
waliowachagua. Baadhi ya wabunge wanafanya vituko hivi huku wakiwa
wanatambua wazi kwamba heshima waliyopewa ni kwenda bungeni kujadili
matatizo ya wananchi ambayo ni mengi kama migogoro ya ardhi. Hili tukio
la jana ni aibu ya mwaka", alisema Nape.
Alisema, muda wanaokuwepo bungeni, wabunge wanapaswa
kuutumia wote kwa hekima busara na uwezo wao wote kujadili namna ya
kuwezesha Watanzania kufikia maisha bora na siyo kuutumia muda huo
kujadili tofauti zao za kisiasa au namna ya kutekeleza malengo yao
binafsi ya vyama vyao.
"Hatua hii ya wabunge wa Chadema kuamua kuzusha
tafrani na kuvunja kanuni za bunge kwa makusudi ni ya hatari sana, hivyo
wananchi wanapswa kujifunza kwamba hawa siyo watu wa kuwapa madaraka.
Tazama hivi sasa bungeni wapo wachache sasa wananchi wakihadaika
wakawachagua na kuwa wengi bungeni patakuwaje? Hili ni fundisho tosha".
alisema Nape.
Alisema, hatua ya Wabunge na viongozi wa Chadema
kulijadili suala la Mkurugenzi wa Usalama wa Chama hicho, Wilfred
Lwakatare kuhusiana na ugaidi huku wakijua kwamba ni suala ambalo lipo
mahakamani, ni la kujaribu kuingilia uhuru wa mahakama kwa makusudi ili
ifikie mahala mahakama itupilia mbali kesi hiyo kwa kigezo cha
kuinngiliwa uhuru wake.
"Haya ni matumzi mabaya ya bunge ambayo yanasukumwa
na viongozi wao ikiwemo kuingilia uhuru wa mahakama, ili hatimaye
ionekane uhuru wa mahakama umengiliwa kuhusiana na kesi hiyo na hatimaye
itupiliwe mbali. Kila mwenye akili anajua kwamba huu ni mkakati malum
wa Chadema", alisema Nape
Mbali na kukizungumzia bungeni suala ya Lwakatare,
Chadema wamekuwa wakilisema pia mitaani, akitoa mfano hatua ya hivi
karibu ya Mbunge wa Singida, Tuntu Lissu kufanya mkutano na waandishi wa
habari kuzungumzia suala hilo na kwamba mbali na kutafuta kesi hiyo
itupwe pia ni juhudi za Chadema kujaribu kusukuma maamuzi ya mahakama.
"Inashangaza sana, Lisu badala ya kutoa ushahidi
wake maghakamani kuhusu suala hili anakwenda kujzungumza na wandishi wa
habari ili hali anafahamu wazi kwamba kesi kuhusiana na suala hilo ipi
mahakamani, tafsiri yake ni kwamba ni juhufdi za Chadema kujaribu
kusukuma maamuzi ya mahakama au kushawishi mahakama kutupilia mbali kesi
kwa kigezo kwamna imeingiliwa uhuru wake", alisema na kuongeza:.
"Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, Freman Mbowe) pia
wakati akizungumza Bungeni alitumia muda mrefu kuzungumzia suala la
Lwakatare lililopo mahakamani. leo mahakama ionekane uhuru wake
umeingiliwa iitupe kesi, na hata wakati wa kuchangia bajeti ya Utumishi,
upande wa Chadema badala ya kuzungumzia sekta ya utumishi wa umma
kurasa nne nzima zilihusu mambo ya Lwakatare", huu ni mkakati mbaya sana
unaolenga haki isitendeke kuhusu kesi hiyo.
Akizungumzia hatua ya Mbunge wa Arusha mjini,
Godbless Lema kutamka bungeni kwamba CCM Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya
Kikwete na Chama Chake cha CCM ndiyo chanzo cha udini, aling'aka kwamba
ni kauli inayotia shaka uelewa wa mambo wa mbunge huyo.
"Nina mashaka kama Lema ni mzima kiakili, CCM
italetaje udini wakati ndiyo imeleta umoja na mshikamano kwa makabila
zaidi ya 24 ya Tanzania kiasi kwamba amani na utulivu vimeshamiri? Yaani
CCM ihangaike kujenga mshikamano halafu hiyo hiyo ione kicefuchefu
kuilinda na kuanza kuihujumu? huu ni upuuzi wa hali ya juu sana",
alisema Nape.
Nape alisema, vituko vyote vinavyoendelezwa na
Chadema Bungeni na kwingineko ni dalili tisha kwamba wanaendelea
kutekeleza ahadi waliyotangaza siku nyingi kwamba nchi haitatawalika.
Mkutano huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana inayoendelea mkoani Morogoro, ambapo pamoja na
Nape, Kinana anafuatana na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohamed Seif
Khatib. Ni ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa ilani ya CCM
mkoani humo.
No comments:
Post a Comment