Ofisa
Mkuu wa Usambazaji na mauzo wa Vodacom Tanzania, Hassan Salleh, akitoa huduma
kwa wateja waliofika wakati wa uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja
lililoko katika mtaa wa India Posta jijini Dar es Salam, Vodacom imezindua
maduka mawili yanayotarajiwa kupunguza msongamano katika maduka mengine ya
kampuni hiyo.
Ofisa
Mkuu wa Usambazaji na mauzo wa Vodacom Tanzania, Hassan Salleh, akimkabidhi
funguo, Meneja Miradiwa Vodacom Tanzania, Sharon Rwekola, mara baada ya
kuzinduliwa kwa duka jipya la kampuni hiyo lililoko mtaa wa India posta jijini
dar es Salaam, Maduka hayo yanatarajiwa kupunguza msongamano kwa wateja wa
kampuni hiyo.
Mkuu wa
kitengo cha Mahusiano ya Umma wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda,
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo.
Taarifa
kwa vyombo vya habari.
Utoaji
wa huduma kwa wateja sekta ya mawasiliano wazidi kukua
• Vodacom yazindua Maduka Mawili ya
huduma kwa wateja.
• Watanzania zaidi kuendelea kupata
huduma za mawasiliano.
Dar
es Salaam, April 18, 2013 … Huku jiji la Dar es Salaam
likiendelea kukua kwa kasi na kushududia ongezeko kubwa la watu kutoka sehemu
mbalimbali, upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii umekuwa ukikabiliwa na
changamoto kadhaa kutokana na kasi ya utoaji huduma kutoendana na kasi ya
ongezeko la watu.
Hivi karibuni wakazi
wa maeneo mbalimbali ya jiji la Dra es Salaam walishududia utolewaji wa elimu
kuhusu mfumo wa mawasiliano wa 3G na 4G mfumo ambao unatumia teknolojia mpya ya
mawasiliano kazi iliyofanywa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Baadhi ya wananchi
waliofikiwa na kampeni hiyo ya utoaji elimu walitoa wito kwa serikali
kushirikiana na wadau wengine wa teknolojia na mawasiliano kutoa elimu juu ya
masuala mbalimbali ya teknolojia na mawasiliano pamoja na matumizi sahihi ya
huduma hizo.
Katika kukidhi haja
hiyo ya utoaji wa huduma kwa wateja na elimu kwa wakazi wa jiji la Dar es
Salaam, Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeendelea kupanua wigo wa
huduma kwa kufungua maduka mawili yatakayo endelea kutoa huduma kwa wateja na
kufanya mauzo ya bidhaa mbalimbali katika mtaa wa India na barabara ya Morogoro
jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia wakati
wa uzinduzi wa maduka hayo, Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya Umma, wa Vodacom
Tanzania Joseline Kamuhanda, amesema Vodacom ni kampuni pekee ambayo imeendelea
kuongoza kwa kuwa na maduka mengi ya mauzo na huduma kwa wateja kwa kufikisha
maduka 65 ikiwa ni kampuni pekee kuwa na maduka mengi ya huduma na kufanikisha
adhma ya kukidhi mahitaji ya huduma kwa wateja wa kampuni hiyo huku Dar es
Salaam ikiwa na idadi ya maduka 20.
“Ukuaji wa huduma kwa
kampuni ya Vodacom umekuwa mkubwa sana, huduma kama ya M – Pesa sasa imepanuka
kwa kasi na sasa inatoa huduma kwa watanzania zaidi ya milioni 10. Kufuatia
mafaanikio haya tunalazimika kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwa wateja ni wa uhakika” alisema Kamuhanda na kuongeza
kuwa,
“Kuongoza katika
sekta ya mawasilaino kuna changamoto zake, lazima tuhakikishe tunaendana na
kasi ya ukuaji na ongezeko la watu na uhitaji wa huduma zetu kwa watu wa aina
mbalimbali.
Aidha Kamuhanda
alisema kuwa Kufunguliwa kwa maduka hayo sasa sio tu kunaboresha upatikanaji wa
huduma pia ni fursa pekee ya kuendelea kupanua wigo wa ajira kwa watanzania.
“Ufunguzi wa maduka
haya unatoa fursa ya ajira kwa Watanzania, Ufunguzi huu umejumuisha na ajira
kwa wafanyakazi 10 ambao watatoa huduma kwa wateja wetu hivyo ni hatua kubwa
tumetengeneza ajira kwa wafanyakazi wapya. Hadi kufikia sasa, Vodacom imetoa
ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi 500 na wengine zaidi ya 30,000 wenye
ajira zisizo za moja kwa moja,”
Kuhusu
Vodacom Tanzania:
Kampuni ya Vodacom
Tanzania ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na jamii katika shughuli za
maendeleo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation. Vodacom Foundation ina
nguzo kuu tatu: Afya, Elimu na Ustawi wa Jamii. Hadi sasa taasisi hiyo
imechangia zaidi ya miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha, imeshinda tuzo
mbalimbali za kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika
kwa Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and Inclusion
Award ambayo hutolewa na kampuni mama ya Vodafone.
Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya simu za
mikononi inayoongoza Tanzania inayotumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano.
Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South
Afritca, ambayo pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty)
Limited inamiliki hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na asilimia 35 zilizobaki
zinammilikiwa na Mirambo Ltd.
Vodacom Tanzania imetangazwa kuwa Super Brand
(Chapa Bora Zaidi) kwa miaka minne mfululizo, kutoka 2009 -2013.
No comments:
Post a Comment