Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia)
akiwa na mshtakiwa mwenzake Saleh Mkadamu wakielekea kupanda basi la
magereza baada ya hukumu ya kesi yao kuahirishwa hadi Mei 9. Sheikh
Ponda Issa Ponda na wenzake 49 wanakabiriwa na makosa matano ya kula
njama na kuingia kwa jinai katika uwanja namba 311/3/4 kitalu T uliopo
Markaz Chang'ombe na wizi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani
ya Shs milioni 59 mali ya kampuni ya Agritanza. (Picha na Habari Mseto
Blog)
Wafuasi
wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa
Ponda wakiwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam leo wakati hukumu ya kesi yake ilipoahirishwa leo.Askari wakiimarisha ulinzi nje ya Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Askari wakiimarisha ulinzi nje ya Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo PICHA ZOTE KWA HISANI YA HABARI MSETO BLOGSPOT.COM
No comments:
Post a Comment