Ligi
ya Mabingwa wa Mikoa kutafuta timu tatu zitakazopanda kucheza Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao chini ya usimamizi wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itaanza Mei 12 mwaka huu.
Mwisho
wa mikoa kuwasilisha majina ya mabingwa wao ni Mei 1 mwaka huu wakati
ratiba ya ligi hiyo itapangwa mbele ya waandishi wa habari Mei 3 mwaka
huu kwenye ofisi za TFF.
Uwasilishaji
wa jina la bingwa wa mkoa unatakiwa kufanyika pamoja na ulipaji ada ya
ushiriki ambayo ni sh. 100,000. Mfumo wa ligi hiyo ni bingwa wa mkoa X
kucheza na bingwa wa mkoa Y nyumbani na ugenini ambapo mshindi ndiye
anayesonga mbele katika hatua inayofuata.
Usajili
wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika hatua ya mkoa na
unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda
kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.
KILA LA KHERI AZAM FC
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Azam
FC katika mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho
dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco itakayochezwa kesho (Aprili 20 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Azam
FC ina fursa nzuri ya kufanya vizuri kwenye mechi hiyo itakayochezeshwa
na mwamuzi Emile Fred kutoka Shelisheli kutokana na maandalizi
iliyofanya, lakini vilevile tunatoa mwito kwa Watanzania kujitokeza kwa
wingi uwanjani kuiunga mkono.
Makocha
wasaidizi wa timu zote mbili, Kalimangonga Ongala wa Azam na Lahcen
Ouadani wa AS FAR Rabat wamezungumza na waandishi wa habari kuhusu mechi
hiyo, kuwa wamejiandaa kuibuka na ushindi.
Kocha
Ongala amesema wamepata DVD za mechi tatu za mwisho za AS FAR Rabat,
moja ikiwa dhidi ya timu ya Al Nasir ya Libya ambayo waliitoa katika
raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho na nyingine mbili za ligi ya
Morocco ambazo wanazifanyia kazi kuhakikisha wanashinda kesho.
Naye
Ouadani amesema hawaifahamu vizuri Azam, lakini wanaujua mpira wa
Tanzania baada ya kuangalia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya
Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) iliyochezwa
jijini Dar es Salaam Machi 24 mwaka huu na Stars kushinda mabao 3-1.
Baadhi
ya wachezaji ambao Azam inatarajia kuwatumia kwenye mechi ya kesho ni
pamoja na Aishi Manula, Mwadini Ally, Khamis Mcha, John Bocco na Salum
Abubakar ambao pia wamo kwenye kikosi cha sasa cha Taifa Stars kilicho
chini ya kocha Kim Poulsen.
AS
FAR Rabat ina wachezaji sita kwenye timu ya Taifa ya Morocco. Wachezaji
hao ni mabeki Younes Bellakhdar, Abderrahim Achchakir, Younnes Hammal,
na viungo Salaheddine Said, Salaheddine Aqqal na Youssef Kaddioui.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment