Friday, April 19, 2013

'BUNGE LA KUPEANA HAKI KWA WASIO NA HAKI'

Na Bryceson Mathias

Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja”. Biblia Mithali 27:1-5.
Ni heri Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe; Mtu mgeni wala si midomo yako wewe!. Jiwe ni zito, na mchanga hulemea; Lakini ghadhabu ya mpumbavu ni nzito kuliko hivi vyote viwili.Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu?. Lawama ya wazi ni heri, Kuliko upendo uliositirika.
Kanuni za Bunge letu, licha ya kwamba linaongozwa na Kiti chenye Ubabe, hazipaswi kuwaona wabunge wengine wana haki na wengine hawana Haki; ila hoja za msingi zijibiwe,na maamuzi yasifanyike kwa mabavu.
Nasema hivyo kwa sababu gani, Kibiblia Utawala wa kizembe wa Kifilisti, Ulimtumia vibaya Delila kwa rushwa ya , Fedha ya Elfu na Mia Moja, na hivyo kuharibu Maisha ya Samsoni kwa kumtoboa Macho, kulikobabisha vifo vya watu ElfuTtatu Waume kwa Wake.
Kiti cha Spika, kwa kukiuka Haki za wenye Haki na kuwapa wasi na Haki, mnataka kutuambia nini?, je mataka maafa na vifo vya wapiga kura na wananchi wao kwa wao wangapi!, Amani itakapokosekana nchini?.
Kaka na Mdogou mtu maskini muda mrefu, walipata bahati kufanya kazi nchi ya ugenini, yenye mshahara mnono na Heshima kubwa, ili waondokane na umaskini na kuwasaidia ndugu zao wakirejea.
Mkuu wa Ukoo, aliwapa ruksa wakafanye kazi kwa sharti la kuisaidia Jamii iondokane na umaskini wa miaka mingi, pindi watakapopata Utajiri.
Kimsingi familia na ukoo mzima ulimuamini sana Kaka mtu kwamba atamuongoza na kumshauri vizuri mdogo wake, kutokana umri wa kutangulia kuzaliwa na kufahamu mengi, kutokana na uzoefu aliokuwa nao akilima vibarua vya kulima Karanga kijijini humo, kiasi cha kuwa na mavazi ya ahueni,, kuliko wengine.
Waliagwa waende kazini,  Kaka akitakiwa amuongoze na kumsaidia mdogo. Kaka alikuwa na Sanduku la Mbao, ambapo kijijini lilionekana lzuri kuliko wengine waliokuwa wakiweka nguo zao kwenye vikapu na kutundika kwenye Kamba.
Mdogo mtu alikuwa na Lambo iliyochanika, ambayo aliweka Mgolole wa Lubega, wakapanda ndege kwa mara ya kwanza uhenini, wakafika.
Walipopata Mshahara wa Kwanza; Mdogo alinunua Sanduku la Matairi na Nguo; zilizobaki aliwanunulia Wazazi na Familia Zawadi na Nguo moja moja akaweka sandukuni, huku kaka mtu akijivunia sanduku la mbao, aliishia kunywa pombe na mzinga wa nyuki.
Mshahara wa pili na watatu, mdogo alijiimarisha kwa kununua vitu mbalimbali walivyoagizwa na familia, kakaye akitesa Kilabuni na wadada. Ghafla tangazo la nchi likawataka wageni kurudi makwao, mdogo alikuwa na Masanduku 10 Nguo na Fedha.
Kwa wapesi wa sanduku wakienda ‘Airport’, kaka akabeba Jiwe kubwa akaweka sandukuni akalifungia. Walipopokewa kijijini, hadhara ilitaka kila mmoja afungue zawadi, mdogo alitoa akashangiliwa na chereko chereko, k kaka alikataa kufungua, wakavunja sanduku na kuona Jiwe akapigwa mawe na ukoo hadi akafa.
Kwa wema Mungu alimrudishia Samson Nguvu (Amuzi.16.28-31), hasira dhidi ya Delila ilipoteza watu maelfu, Mali na Makazi  kwa hasira. Je, Naibu Spika Job Ndugai, hicho kiti utakalia wewe tu Milele?Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja, unaweza ukakosa Ubunge 2015!. Utajisifu kwa nani?
nyeregete@yahoo.co.uk. 0715-933308

No comments:

Post a Comment