Kampuni ya Ijumba Enterprises kuzindua mradi huu unaomgusa
kila mmoja wetu mwanzoni mwa mwezi wa kumi na moja kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi Kitengo cha
usalama Barabarani na Chuo cha Usafirishaji cha Taifa(NIT) Kuzindua mradi wa uitwao SAFER JOURNEY
(SAFIRI SALAMA) Mwanzoni mwa mwezi wa 11 / 2013 Wenye lengo la kupunguza Ajali za pikipiki
barabarani (Boda Boda) ambazo si za
lazima kwa watumiaji wa pikipiki, Kwa kuongeza ufahamu wa matumizi ya barabara
kupitia semina,warsha,vipindi vya Redio na TV.
Pia Ijumba Enterprises imegundua kuwa Boda boda walio
wengi ni chini ya miaka kumi na nane
hivyo hawana leseni ya kuendeshea vyombo hivyo vya moto, kupitia mradi huu
vituo vyoote vya Bodaboda na uongozi wake lazima visajiliwe na vitambuliwe na
mamlaka husika, pia Bodaboda lazima wawe na vitambulisho, Vitambulisho hivyo
vitatolewa kwa dereva wa pikipiki mwenye leseni ya kuendeshea pikipiki halali.
Kwa pamoja tunaweza kuepusha Ajali za pikipiki ambazo si za lazima.
Endesha kwa
usalama Epusha Ajali. Tunapatikana Face book,Twitter, na Skype. Email: safejourneyproject@gmail.com.
0754 038 158 / 0655 038 158
No comments:
Post a Comment