Saturday, March 31, 2012

TUZO ZA UMAHIRI KATIKA UANDISHI WA HABARI MWAKA 2011 (EJAT) WAFAANA.

Rais JakayaKikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Baraza la Habari Tanzania,(MCT) wapili kushoto ni Waziri wa Habari Vijana na Michezo Tanzania Dk.Emmanuel Nchimbi,wa Nne ktoka kushoto ni Mwenyekiti wa MCT Dk.Justice Robert Kisanga,Naibu Mwenyekiti Chonde Omary,Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Kajubi Mukajanga.
Fili Karashani (kushoto) akiwa na mwanae huku akimuonyesha Tuzo ya Maisha ya ufanisi katika tasnia ya habari iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), katika hafla ya kuwatunuku waandishi wa habari bora wa mwaka 2011. tuzo hiyo ilikuwa ikishindaniwa na Eda Sanga na Ben Kiko.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda (Kulia) akimkabidhi Tuma Dandi wa Mlimani Radio tuzo ya ushindi wa uandishi wa habari za walemavu katika hafla iliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Baadhi ya majaji wakifuatilia shughuli nzima ya utoaji wa tuzo kwa waandishi wa Habari,kutoka kushoto ni Bernadina Chahaki wa DTV ,Mwanzo Milinga na Attilio Anselm.
Rais Jakaya Kikwete akitetw jambo na Mwenyekiti wa Ipp Regnard Mengi wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa waandishi wa habari bora 2011. iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT)

No comments:

Post a Comment