Monday, April 2, 2012

KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA MASHIRIKA YA UMMA (POAC) YATEMBELEA OFISI ZA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA.

Jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania lililopo katika eneo la Sinza , barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam, likiwa katika muonekano wa kisasa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Mawasiliano TCRA ,Profesa John Mkoma, akifafanua jambo kwa wanakamati wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) wakati walipotembelea katika ofisi za TCRA jijijini Dar es Salaam, wa pili kutoka mkulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Philip Njombe.
Meneja wa Utafiti na Mipango wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dk.Ally Simba akiwaonyesha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) kifaa kinachotumika kupimia miozi ya minara ya simu, ambayo wengi wamekuwa wakisema kuwa inaathari kwa binadamu,wakati walipotembelea katika Ofisi za TCRA, kujionea shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo.
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC ) akiuliza swali kuhusiana na shughuli za Mamlaka ya Mawasiliano.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Mawasiliano TCRA ,Profesa John Mkoma, akifafanua jambo kwa wanakamati wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) wakati walipotembelea katika Ofisi za TCRA jijijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Philip Njombe na mjumbe wa kamati hiyo Bi, Felista Bura.

No comments:

Post a Comment