Monday, April 9, 2012

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ALIVYOKWENDA KUHANIKATIKA MSIBA WA STEVEN KANUMBA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiakisaini kitabu cha maombolezo katika msiba Inspekta Jenerali wa Polisi Mstaafu Marehemu Harun Mahundi aliyefariki april 5, 2012 na kuzikwa jana jijini Dar es salaam.

Rais Kikwete akiaga waombolezaji nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam April 8, 2012 alikofika kuomboleza nao kifo hicho.

Rais Kikwete akiongea na wanakamati ya msiba wa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam, April 8, 2012 alikofika kuomboleza nao kifo hicho.

Rais Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam, April 8, 2012 kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wafiwa.

No comments:

Post a Comment