Monday, June 25, 2012

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YAKE YA JIUNGE NA SUPA5 JIJINI MWANZA,

 Meneja Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Tanzania,Jackson Mmbando akimkabidhi Jamila Juma simu ya mkononi aina ya Sumsung,baada kuibuka mshindi kwa kuichammbua vyema huduma mpya
ya Airtel Jiunge na Supa5.
 Jamila Juma na  Sandra Mwashitete wakipewa maelekezo mafupi namna ya kutumia mtandao wa Airtel pamoja na huduma zake mbalimbali, mara baada ya kujishindia simu aina ya Sumsung,wakati kampuni ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Jiunge na Supa5,uliofanyika jana kwenye viwanja vya Furahisha,jijini Mwanza.
Juma Nature msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya na kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi kutoka Temeke,jijini Dar,akiwa sambamba na msanii mwenzake (hayupo pichani) aitwaye Kr-Mulla wakilishambulia jukwa huku shangwe kubwa ikilipuka kutoka kwa sehemu kubwa ya wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.

No comments:

Post a Comment