Tuesday, June 5, 2012
TUNASUBILI KUONA UWEZO WA WAKUU WA WILAYA .
HIVI karibuni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alifanya mabadiliko ya uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya nchini kwa lengo la kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo.
Tunaipongeza Serikali kwa kufanya hilo kutokana na baadhi ya wakuu wa wilaya walikuwa wapo nyuma katika kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo na kuachia madaraka kwa viongozi wengine waweze kusimamia.
Hali hiyo ilikuwa ikifanya inaleta maswali mengi hivi mkuu wa wilaya anashughuli gani katrika wilaya husika ikiwa kazi zake zinafanywa na mtu mwingine wakati huo huo mshahara anapokea kama kawaida?
Pengeni wakati wa mchujo huo nadhani suala hilo limekuwa likiangaliwa kwa umakini kutokana na wananchi wengi wamekuwa wakitoa malalamiko hawana imani na viongozi wao mabo ni wakuu wa wilaya.
Naamini kwa baadhi ya wilaya ambazo wananchi walikuwa wakitoa malalamiko ya watendaji wao ambao ni wakuu wa wilaya na kuondolewa kabisa katika madaraka wamefurahi na kwa upande mwingine bado wana dukuduku kwa kurejeshwa kwa mkuu wa wilaya wa zamani.
Nimekuwa shuhudu kwa kupitia vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikiripoti taarifa nyingi kuhusu wanannchi kuwakataa wakuu wao wa wilaya ambao awali walikuwa wakiongoza na kurejeshwa kwa mara nyingine waweze kulisukuma gurudumi hilo.
Tukiachana na hilo hali hiyo imekuwa ikitokea katika maeneo mabalimbali kuwepo na watendaji wabuvu katika kuhakikisha wanasimamia maendeleo ya miradi ya wanannchi wake katika wilaya husika.
Pia jukumu lingine ni pamoja na kuhakikisha kuwa maeneo yao yanakuwa na miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa viwango stahiki na nidhamu katika ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za umma na kujiridhisha kuwa zinatumika kwa manufaa ya wananchi.
Kadhalika jukukumu lingine ni pamoja na kuhakikisha wanasimamia vizuri ukusanyaji wa mapato kwenye halmashauri zao kwa sababu ndiko viliko vyanzo vikuu vya mapato.
Katika bajeti iliyopita, halmashauri zilipanga kukusanya Sh320 bilioni lakini, hadi kufikia Januari mwaka huu, ni Sh90 bilioni tu ambazo zilikuwa zimekusanywa, na hali hiyo imetokana na kuwepo kwa usimamizi mbovu kwa baadhi ya watendaji katika Halmashauri hizo.
Aidha jukumu lingine ni kuhakikisha kuwa mikoa na wilaya zao zina akiba ya chakula cha kutosha na kuwa na fursa za kuzalisha mazao mbadala , na kumizeni watu wao walime mazao yanayostahimili ukame, yanayokomaa kwa muda mfupi na hata kuwasisitiza wazalishe chakula cha ziada ili wawe na akiba ya kutosha na pia waweze kuuza na kupata fedha.
Kilichonifanya kuandika suala hili pamoja na wananchi wa wilaya ya Iramba wamekuwa wakitoa malalamiko yao inakuwaje mwanafunzi wa chuo Kikuu Finland ambaye anatarajia kumaliza masomo yake mwaka 2014. ambaye kachaguliwa kuwa mkuu wa wilaya.
Kutokana na hivi sasa yupo masomoni na bado ana miaka miwili ya kumaliza je kwa muda huo nani atakuwa anafanya yale majukumu yake na mshahara atalipwa wakati yupo huko? Na hata hivyo sasa hapa kuna maswali mengi yanakuja watajigawa vipi katika kusimamia miradi ya maendeleo ya wananchi?
Hata nilipata fursa ya kusikiliza majibu ya mkuu huyo katika mahojiano ya Televisheni ya TBC1 alisema kuwa ataweza kuugawa muda wake ili kuhakikisha wananchi wanapata waki zao za msingi na yeye anajipatia haki yake ya kupata elimu.
La asha kulingana na majibu yake sikuweza kupata jibu la haraharaka na kuanza kujiuliza muda gani atakaoutenga kwa ajili ya kusimamia miradi ya maendeleo na kuwatumikia wananchi wake akiwa huku nje.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment