Saturday, October 13, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AOMBOLEZA KIFO CHA MFANYAKAZI WA OFISI YAKE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa mfanyakazi katika Ofisi yake ya jijini Dar es Salaam, Jenkins Chochole Matulile, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita jijini. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifanyika nyumbani  kwao Mbezi Tangi Bovu na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam  Picha na OMR
-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe, Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu,  Jenkins Chochole Matulile, aliyekuwa mfanyakazi katika Ofisi yake ya jijini Dar es Salaam, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita jijini. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifanyika nyumbani  kwao Mbezi Tangi Bovu na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam leo, Oktoba 11, 2012.

No comments:

Post a Comment