Monday, October 29, 2012

Waamuzi wanne waondolewa fainali za AWC

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewarejesha nyumbani waamuzi wasaizidi wanne waliokuwa wameteuliwa kuchezesha fainali za Nane za Afrika kwa Wanawake (AWC) zinazoanza kesho (Oktoba 28 mwaka huu jijini Malabo, Equatorial Guinea.
 
Kwa mujibu wa Meneja wa Waamuzi wa CAF,  Bester Kalombo waamuzi hao wamerejeshwa nyumbani baada ya kushindwa mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) uliofanyika jana (Oktoba 26 mwaka huu).
Waamuzi hao ni Emmanuella Aglago kutoka Ghana, Atallah Mona Mahmoud wa Misri, Mary Njoroge (Kenya) na Nchama Edu Manuela wa Equatorial Guinea.
 
Kalombo alisema baada ya hao kuondolewa wameongeza waamuzi wasaidizi wengine wawili ili kuziba nafasi zao. Waamuzi wasaidizi walioongezwa ambao walikuwa kwenye orodha ya akiba ni Marthe Sakobo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Mercy Zulu wa Zambia.
 
Waamuzi wa kati walioteuliwa kuchezesha fainali hizo na ambao wote walifaulu mtihani huo ni Aissatta Amegee (Togo), Christine Ziga (Ghana), Gladys Lengwe (Zambia), Grace Msiska (Malawi), Incaf El Harkaoui (Morocco), Kankou Coulibaly (Mali), Ledia Tafese (Ethiopia), Maximina Luzia Bernado (Angola), Nabikko Ssemambo (Uganda), Naema Rashad Mohamed (Misri) na Therese Sagno (Guinea).
 
Kwa upande wa waamuzi wasaidizi waliofuzu ni Adijat Bosede Momo, Bernadettar Kwimbira (Malawi), Botsalo Watlala Mosimane (Botswana), Diana Junia Mukasa (Uganda), Lidwine Rakotozafinoro (Madagascar), Mana Ayawa Dzodope (Togo), Marthe Gamoeda Laconte (Jamhuri ya Afrika ya Kati), N’dah Francois Tempa (Benin), Souad Oulhaj (Morocco), Trhas Gebreyohanis (Ethiopia) na Tseke Ngouono (Congo Brazzaville).
 
Boniface Wambura, Malabo, Equatorial Guinea
+240 222132743

No comments:

Post a Comment