Saturday, October 27, 2012

Wateja wa Airtel sasa kulipia Kodi kwa Airtel Money


Mwakilishi wa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Saleh Mshoro (kulia), Mkurugenzi wa Biashara za Mashirika wa Airtel, Irene Madeje (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Allan Kiula (kushoto) wakionyesha moja ya kipeperushi kinachoelekeza namna ya kulipa kodi wakati wa uzinduzi wa huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipa Kodi ya Mapato na Majengo kwa kupitia Huduma ya Airtel Money. Uzinduzi huu ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Makao Makuu ya Ofisi za Airtel Morocco jijini Dar es Salaam. (Picha  kwa hisani ya Airtel)

Mkurugenzi wa Biashara za Mashirika wa Airtel bi Irene Madeje Mlola (Kulia) akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipa kodi ya mapato na Majengo kwa kupitia Huduma ya Airtel Money,pichani katikati ni Mwakilishi wa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania bw Saleh Mshoro akiongea na kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi bwn Allan Kiula.


*Wateja wa Airtel sasa kulipia Kodi kwa Airtel Money*

**Kulipia kodi ya mapato na majengo *

**Airtel na TRA kuwezesha ukusanyaji na ongezeko la mapato *

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma za mawasiliano yenye gharama nafuu zaidi na mtandao wenye wigo mpana leo imezindua mwendelezo wa huduma za Airtel kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwawezesha wateja wake nchi nzima kulipia Kodi kupitia huduma ya Airtel Money. Hii imekuja wakati huduma za pesa kutumia simu zimekuwa zikibadilisha huduma za kibiashara na kuongeza ufanisi.

Kwa kupitia huduma ya Airtel money na ushirika na Mamlaka ya Mapato
Tanzania Airtel wateja wa makampuni hayo wataweza kulipia kodi ya mapato na majengo kupitia Airtel Money.


Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika makao makuu ya kampuni ya Airtel,
Mkurugenzi wa Biashara za Mashirika bi Irene Madeje Mlola alisema” Airtel
imekuwa mstari wa mbele katika kuleta ufanisi na mapinduzi katika sekta ya
mawasiliano nchini. Leo tuna furaha kushirikiana na Mamlaka ya Mapato

Tanzania (TRA) kwa kuwezesha wateja wake kulipa kodi kwa kupitia huduma yaAirtel Money.

Airtel money ni huduma iliyotengezwa kukithi mahitaji ya
wateja wetu na hii ni hatua nyingine muhimu kwa Airtel kutumia miundo mbinu tuliyonayo na TRA katika kuhakikisha wanaboresha huduma zao. Sasa walipaji wa kodi wadogo na wakubwa wanalipia kodi zao kwa urahisi wakiwa katika biashara zao na nyumbani”

“Mpaka sasa takribani nusu ya wateja wa Airtel wamejiunga na kutumia huduma ya Airtel money, huduma iliyo rahisi, iliyojitosheleza, salama na nyenye kutoa nafasi kufanya miamala mbalimbali ikiwemo malipo ya bidhaa

mbalimbali. Kwa kupitia huduma ya Airtel money inayotoa huduma nyingi zaidi ya kutuma pesa tumeona maisha ya watanzania wengi yakibadilika kila siku na biashara zao kuwa na ufanisi zaidi aliongeza Madeje.”

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania bwRished Bade alisema” Tunayofuraha kuzindua huduma yenye kutumia mfumo wa teknolojia ya malipo ya uhakika na salama kwa wateja wetu nchi nzima.

Uzinduzi wa leo ni udihirisho wa juhudi za Mamlaka katika kuongeza

uboreshaji katika huduma za malipo ya kodi na ukusanyaji wa
mapato.Tunategemea kwa kupitia huduma ya Airtel Money kutawezesha ulipaji wa kodi kwa wakati na kuwahamasisha watanzania wengi zaidi kulipia kodi zao za mapato na majengo. TUnategemea kuona ongezeko kubwa la wafanya biashara wadogo na wakati ambao leo hii wanalipia malipo ya kodi kwa kupitia maofisi na vituo mbalimbali vya kodi nchi nzima.

Akiongelea kuhusu njia ya kulipia kodi hizo kwa njia ya simu Meneja
Uendeshaji Airtel Money Asupya Naligingwa alieleza”Kulipia kodi ya majengo

au mapato mteja wa Airtel atatakiwa kupiga namba  **150*60#*  kisha

   1. Atachagua Lugha
   2. Atachagu malipo ya bili
   3. Lipa Bili

   4. Atachagu “JIna la fumbo” MAJENGO”
   5. Ingiza kiasi cha fedha unachotaka kulipia
   6. Ingiza neno la siri
   7. Ingiza namba ya akaunti ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kisha bonyeza OK

   na utapokea meseji(SMS)itakayothibitisha malipo yako ”

Huduma ya Airtel Money service inayopatikana kwa kupiga  **150*60# *
inawawezesha  

wateja kulipia huduma mbalimbali zikiwepo kama vile za kulipia bili za maji 
na umeme,bidhaa na huduma mbalimbali kama vile  bima,kununua muda wa 
 vile vile kulipia huduma nyingine nyingi. maongezi,miamala ya huduma za kibenkiikiwemo kuweka na kupokea kutoa na
Airtel Money ni huduma inayopatikana masaa 24, siku 7 za wiki kutoka katika
simu na ni salama ya uhakika na rahisi kutumia. Kinachohitajika ni
kitambulisho na usajili wa simu yako ili kuweza kupata huduma hii katika
maduka na mawakala wote waliopo nchi nzima.

No comments:

Post a Comment