Monday, January 7, 2013

MAMBO YA MTWARA NA LINDI.

 Kukithiri kwa vifo na majeraha kwa waendesha pikipikio katika  mkoa wa Mtwara,  Jeshi la Polis kitengo cha usalama barabarani kimeanza kutoa elimu kwa madereva na wamiliki ili kupunguza ajari zinazo sababisha msongamano hospitalini. Pichani ni mmoja wa mafundi wa pikipiki akinyosha ringi eneo la viwanja vya Mashujaa.
 Muuguzi  Mkuu  wa Hospitali  ya rufaa ya Sokoini  mkoa wa Lindi Beatrice Mkwela akionyesha  baadhi ya vifaa vitakavyotumiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi wa  katika hospitali hiyo. Wodi hiyo inatarajiwa kufungukliwa mwishoni mwa mwazi huu.
 
 .Kijana ambaye jina lake halikupatikana akiendesha baiskeli katika barabara ya mingumbi eneo la ufukwe wa Lindi mjini huku akiwa amebeba gogo begani kwake.
 Baadhi ya majeruhi wa ajari za pikipiki maalufu kama bodaboda wakiwa wamelazwa katika wodi ya wagonjwa  katika hospitali ya  Ligula mkoa wa Mtwara .Ajari za pikipiki zimekuwa tishio la nguvu kazi za vijana mkoani humo jambo ambalo limiwalazimu jeshi la polisi kuanza kutoa elimu juu ya uendeshashi wa pikipiki ikiwemo uvaaji wa Kofia ngumu.

 Mmoja wa wanamgambo wa halmashauri ya mkoa wa Lindi akiwaswaga ng’ombe baada ya kuwakamata wakizagaa katikati ya mji huo hivi karibuni.
 BILA KOFIA HAKUNA SAFARI ;Mwendesha pikipiki katika mkoa wa Mtwara akiwa amempakia abiria hukua wakiwa wa mevaa kofia ngumu ,Jeshi la polisi  usalama wa barabarani limefanikiwa kwa kiasi kikubwa  kutoa elimu juu ya uvaajiwa kofia hizo.

No comments:

Post a Comment