Mtafiti wa Masoko ya Ajira, VETA Makao Makuu Julius Paul Mjelwa akitoa maelezokwa wageni waliotembelea banda la VETA kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), kuhusu huduma na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na vyuo vya VETA.
.Mhandisi Adrian Kashula wa VETA Kipawa jijini Dar es Salaam, akitoa maelezo kuhusu teknolojia ya kisasa ya umeme wa viwandani ambayo inatumia eneo dogo na kutoa taarifa pale panapotokea hitilafu, akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda hilo.
Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa VETA Chang’ombe Dar es Salaam, fani ya uchoraji ramani na usanifu majengo, Fatma Mohamedi akitoa maelezo kuhusu mafunzo ya taaluma hiyo yanayotolewa na chuo hicho katika ngazi mbalimbali.
Baadhi ya mashine na mitambo inayozalishwa na vyuo mbalimbali vya VETA nchini,ambayoikitumika vema inaweza kulikomboa taifa kiuchumi kwa kuepuka utegemezi wa mashine na mitambo kutoka nje.
Unajua sauti inaweza kutumika kuzalisha umeme? Fika banda la VETA katika Maonyesho ya Sabasaba ujionee teknolojia hiyo. Pichani Mkufunzi wa Ufundi Sirili Aloyce akionyesha mojawapo ya mashine hizo na namna inavyofanya kazi. Huo ni miongoni mwa ugunduzi na utafiti uliofanywa na VETA.
.Matumizi ya dizeli na petrol kuzalisha umeme kutumia jenereta sasa basi. VETA imekuja na teknolojia ya kuzalisha umeme kwa kutumia betri, hivyo kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya dizeli na petrol. Mwanafunzi wa VETA wa Mitambo na Mashine, Emmanuel Ngowo akionyesha jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.
.Kwanini tunedelea kuuza ngozi ghafi nje? VETA wamekuja na jibu kupitia Chuo chao cha Dakawa, Morogoro kinachotoa mafunzo ya usindikaji na uzalishaji wa bidhaa za ngozi vikiwemo viatu vya aina mbalimbali. Mwanafunzi wa VETA Onesmo Mrisho akitoa maelezo jinsi wanavyozalisha bidhaa za ngozi.
Hawaamini, kisha wakafurahi baada ya kupata maelezo kuhusu mafunzo ya hoteli na utalii yanayotolewa na vyuo vya VETA vya Dodoma na Njiro mkoani Arusha. Pichani Mwanafunzi Theopista Michael akitoa maelezo wa wageni waliotembelea banda la VETA katika maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment