Mkurugenzi wa Sekta ya Wachangiaji na Watoa Huduma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Dkt. Raynold Mfungahema akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa mitandao (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,,jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali hapa nchini wakiwa kazini wakati wa warsha ya bloggers iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Profesa John Nkoma akitoa mada ya sekta ya mawasiliano Tanzania wakati wa warsha ya wamiliki wa blogger hapa nchini iliyoandaliwa na TCRA.
Baadhi ya wamiliki wa (mitandao)bloggers wakiwa katika warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania wakiweka habari za katika mitandao yao .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tech-Walk, Liz Wachuka akitoa mada katika wasrsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. (TCRA)
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Profesa John Nkoma akijibu swali aliloulizwa na mmoja wa washiriki wa warsha ya blogger iliyoandaliwa na TCRA.
Mtendaji Mkuu wa Google Afrika Joe Mucheru akitoa mada ya ufanisi wa Blogs kama sehaemu ya vyoma vya Jamii wakati wa Warsha ya Bloggers iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. (TCRA)
Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakifuiatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa katika warsha hiyo.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Doris Saivoye akiongea na washiriki wa warsha ya wamiliki wa Bloggers na Mitandaao ya Kijamii Twiter,Facebook.na Yutubu .Warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.jijini Dar es Salaam, ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wamiliki hao. Katikati ni Mkurugenzi wa Google Afrika Joseph Mucheru na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tech-Walk, Liz Wachuka.
No comments:
Post a Comment