Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lamadi kwenye
Viwanja vya Kisesa wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu na kuwaambia
wananchi kuwa muda wa walimu kuendelea kupata tabu umeisha na kuagiza
mamlaka husika kutatua kero na madai ya walimu ndani ya miezi sita na
kama wameshndwa wajiuzulu kupisha watu wengine.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lamadi
wilayani Busega kwenye Mkutano wa hadhara na kuwaambia wananchi wawe
makini na makanjanja wa kisiasa ambao kwa sasa wamefunga ndoa batili
kutaka kuvuruga mchakato wa kupata Katiba mpya.
RAIS KIKWETE AKUTANA NA UONGOZI WA CCM DMV JIJINI WASHINGTON D.C.
Viongozi CCM DMV wakijadiliana jambo kabla ya kikao cha Faragha na
Mhe. Rais Kikwete leo Sept 19,2013 jijini Washington DC, Marekani. Picha
na Swahilitv
Picha na Swahilitv
Mh.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete Mwenyekiti CCM Taifa akielekeza jambo katika
kikao chake na uongozi wa CCM DMV. Kikao hiki kimefanyika leo Sept
19,2013 jijini Washington DC, Marekani. Picha na Swahilitv
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimsalimia Bwana George Sebo mwenyekiti wa CCM DMV.Picha na Swahilitv
Mhe.
Rais Kikwete akiwa na Bwana DMK Mkurugenzi wa MMK MEDIA GROUP: Swahili
TV, Swahili Radio na Swahilitv Blog. Picha zote na Swahili TV.
JWTZ LATOA UFAFANUZI KUHUSU AJIRA
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N
G O M E” Makao Makuu ya
Jeshi,
Telex :
41051 DAR ES SALAAM,19 Septemba,
2013.
Tele Fax :
2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti :
www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
linapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa taarifa zilizoenea kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za
mkononi (sms) na mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba JWTZ limeanza
kuajiri wataalamu Jeshini (Professionals) siyo kweli na halina
utaratibu wa kutangaza ajira kupitia mitandao ya kijamii au kupitia simu za
mikononi.
Kwa
kawaida, utaratibu wa kujiunga na Jeshi hutangazwa kwenye Vyombo vya Habari pale
ambapo Jeshi linahitaji kuandikisha askari wapya. JWTZ huelekeza utaratibu wa kuzingatia katika
kuwasilisha maombi husika kwa taarifa hii, wananchi wote wanatahadharishwa
kuhusu ujumbe huo unaoelekea kusababisha usumbufu kwa wananchi na JWTZ. Taarifa hiyo haijatolewa na JWTZ hivyo
wananchi wajihadhari na yeyote atakayejitokeza kuwarubuni na hatimaye kutapeliwa
kwa namna yoyote.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari
na Uhusiano
Makao Makuu ya
Jeshi
Dar es salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment