Friday, September 20, 2013

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AHUTUBIA WAKAZI WA LAMADI MKOA WA SIMIYU.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lamadi kwenye Viwanja vya Kisesa wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu na kuwaambia wananchi kuwa muda wa walimu kuendelea kupata tabu umeisha na kuagiza mamlaka husika kutatua kero na madai ya walimu ndani ya miezi sita na kama wameshndwa wajiuzulu kupisha watu wengine.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lamadi wilayani Busega kwenye Mkutano wa hadhara na kuwaambia wananchi wawe makini na makanjanja wa kisiasa ambao kwa sasa wamefunga ndoa batili kutaka kuvuruga mchakato wa kupata Katiba mpya.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA UONGOZI WA CCM DMV JIJINI WASHINGTON D.C.

   Viongozi CCM DMV wakijadiliana jambo kabla ya kikao cha Faragha na Mhe. Rais Kikwete leo Sept 19,2013 jijini Washington DC, Marekani. Picha na Swahilitv
Picha na Swahilitv
 Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete Mwenyekiti CCM Taifa akielekeza jambo katika kikao chake na uongozi wa CCM DMV. Kikao hiki kimefanyika leo Sept 19,2013 jijini Washington DC, Marekani. Picha na Swahilitv
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimsalimia Bwana George Sebo mwenyekiti wa  CCM DMV.Picha na Swahilitv
Mhe. Rais Kikwete akiwa na Bwana DMK Mkurugenzi wa MMK MEDIA GROUP: Swahili TV, Swahili Radio na Swahilitv Blog. Picha zote na Swahili TV.

JWTZ LATOA UFAFANUZI KUHUSU AJIRA

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo  : “N G O M E”                Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo  :                              DSM  22150463  
                                                                     Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                            DAR ES SALAAM,19                                                                Septemba, 2013.
Tele Fax                                         : 2153426
Barua pepe          : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                       : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa taarifa zilizoenea kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mkononi (sms) na mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba JWTZ limeanza kuajiri wataalamu Jeshini (Professionals) siyo kweli na halina utaratibu wa kutangaza ajira kupitia mitandao ya kijamii au kupitia simu za mikononi.
          Kwa kawaida, utaratibu wa kujiunga na Jeshi hutangazwa kwenye Vyombo vya Habari pale ambapo Jeshi linahitaji kuandikisha askari wapya.  JWTZ huelekeza utaratibu wa kuzingatia katika kuwasilisha maombi husika kwa taarifa hii, wananchi wote wanatahadharishwa kuhusu ujumbe huo unaoelekea kusababisha usumbufu kwa wananchi na JWTZ.  Taarifa hiyo haijatolewa na JWTZ hivyo wananchi wajihadhari na yeyote atakayejitokeza kuwarubuni na hatimaye kutapeliwa kwa namna yoyote.
                       
Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi

Dar es salaam, Tanzania

MAMLAKA YA MAWASILIANO ILIVYOTOA ELIMU KWA BROGGERS KATIKA WARSHA YA SIKU MBILI JIJINI DAR ES SALAAM.

 Liz Wachuka akitaoa mafunzo kwa wanabloggers wakati wa Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
 Bwana Alex wa Jamii Forums akitoa mada wakati wa Warsha hiyo.


 Pili Mtambalike wa MCT akitoa mada wakati wa Warsha ya Bloggers .
 Baadhi ya wanamitandao( Bloggers ) mbali mbali hapa nchini  wakiwa kwenye Warsha hiyo ya siku mbili iliyofanyik kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akiwasilisha mada ya kwanza juu ya Ukubwa wa Sekta ya Mawasiliano hapa nchini wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi  kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.

 Bwana Benard Rwebangila akikabidhiwa Cheti na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa John Nkoma.

 Mmiliki wa Mtandao wa Mbeye yetu naye hakuwa nyuma akikabidhiwa cheti na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,Profesa John Nkoma.kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akifafanua jambo wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.

 Bashiri Nkoroma ambaye anamiliki mtandao wa chachandu blogs .com akikabidhiwa cheti na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tanzania Profesa John Nkoma.
 Dada la nguvu Shamimu akibidhiziwa cheti na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi.
 Mmiliki wa mtandao wa Father Kidevu Mroki Mroki akikabidhiwa cheti cha kuhitimu mafunzo hayo na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa John Nkoma.
 Mmiliki wa Blogs hii ya Pwaniraha2news.blogs Albart Jackson akikabidhiwa cheti na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.Profesa John Nkoma
 M
 Jef Msangi Bongo akitoa shukrani kwa niaba ya wanabloggers kwa uongozi wa TCRA.
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano akiteta jambo na Mwanzilishi wa Mtandao wa Jamii Forums Mike Mushi.


Tuesday, September 17, 2013

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA)IMETOA MAFUNZO KWA WAMILIKI WA MITANDAO YA KIJAMII IKIWA NI SEHEMU YA KUWAPA UWEZO NA UELEWA WA KUIELIMISHA JAMII KUPITIA MITANDAO .

  Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi akitoa utaratibu  wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamiliki wa mitandao (Bloggers) hapa nchini,Warsha hiyo imeanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam na itamalizika kesho na washiriki watakabidhiwa vyeti vya ushiriki.
 Mkurugenzi wa Sekta ya Wachangiaji na Watoa Huduma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Dkt. Raynold Mfungahema akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa mitandao (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,,jijini Dar es Salaam.

 Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali hapa nchini wakiwa kazini wakati wa warsha ya bloggers iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Profesa John Nkoma  akitoa mada ya  sekta ya mawasiliano Tanzania wakati wa warsha ya  wamiliki wa blogger  hapa nchini iliyoandaliwa na TCRA.

 Baadhi ya wamiliki wa (mitandao)bloggers wakiwa katika warsha ya siku mbili  iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania wakiweka  habari za katika mitandao yao .

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tech-Walk, Liz Wachuka akitoa mada katika wasrsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. (TCRA)
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Profesa John Nkoma akijibu swali aliloulizwa na mmoja wa washiriki wa warsha ya blogger iliyoandaliwa na TCRA.
 Mtendaji  Mkuu wa Google Afrika Joe Mucheru akitoa mada ya ufanisi wa Blogs kama sehaemu ya vyoma vya Jamii wakati wa Warsha ya Bloggers iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. (TCRA)
 Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakifuiatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa katika warsha hiyo.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano  Tanzania (TCRA) Doris Saivoye  akiongea na washiriki wa warsha ya wamiliki wa Bloggers  na Mitandaao ya Kijamii Twiter,Facebook.na Yutubu .Warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.jijini Dar es Salaam, ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wamiliki hao. Katikati ni Mkurugenzi wa Google Afrika Joseph Mucheru na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tech-Walk, Liz Wachuka.

Saturday, June 29, 2013

VETA WALIVYOTHAMILIA KUWAKOMBOA WANANCHI KUPITA MAFUNZO MBALIMBALI,


Mtafiti wa Masoko ya Ajira, VETA Makao Makuu Julius Paul Mjelwa akitoa maelezokwa wageni waliotembelea banda la VETA kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), kuhusu huduma na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na vyuo vya VETA.

.Mhandisi Adrian Kashula wa VETA Kipawa jijini Dar es Salaam, akitoa maelezo kuhusu teknolojia ya kisasa ya umeme wa viwandani ambayo inatumia eneo dogo na kutoa taarifa pale panapotokea hitilafu, akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda hilo.

Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa VETA Chang’ombe Dar es Salaam, fani ya uchoraji ramani na usanifu majengo, Fatma Mohamedi akitoa maelezo kuhusu mafunzo ya taaluma hiyo yanayotolewa na chuo hicho katika ngazi mbalimbali.

Baadhi ya mashine na mitambo inayozalishwa na vyuo mbalimbali vya VETA nchini,ambayoikitumika vema inaweza kulikomboa taifa kiuchumi kwa kuepuka utegemezi wa mashine na mitambo kutoka nje.

Unajua sauti inaweza kutumika kuzalisha umeme? Fika banda la VETA katika Maonyesho ya Sabasaba ujionee teknolojia hiyo. Pichani Mkufunzi wa Ufundi Sirili Aloyce akionyesha mojawapo ya mashine hizo na namna inavyofanya kazi. Huo ni miongoni mwa ugunduzi na utafiti uliofanywa na VETA.

.Matumizi ya dizeli na petrol kuzalisha umeme kutumia jenereta sasa basi. VETA imekuja na teknolojia ya kuzalisha umeme kwa kutumia betri, hivyo kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya dizeli na petrol. Mwanafunzi wa VETA wa Mitambo na Mashine, Emmanuel Ngowo akionyesha jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.

.Kwanini tunedelea kuuza ngozi ghafi nje? VETA wamekuja na jibu kupitia Chuo chao cha Dakawa, Morogoro kinachotoa mafunzo ya usindikaji na uzalishaji wa bidhaa za ngozi vikiwemo viatu vya aina mbalimbali. Mwanafunzi wa VETA Onesmo Mrisho akitoa maelezo jinsi wanavyozalisha bidhaa za ngozi.

Hawaamini, kisha wakafurahi baada ya kupata maelezo kuhusu mafunzo ya hoteli na utalii yanayotolewa na vyuo vya VETA vya Dodoma na Njiro mkoani Arusha. Pichani Mwanafunzi Theopista Michael akitoa maelezo wa wageni waliotembelea banda la VETA katika maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.